Yaliyojiri katika kongamano la Viongozi wa dini Kigamboni kuelekea uchaguzi mkuu 2020
Na Mwamba wa habari
Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni Abdallah Iddi Ally ,kuelekea uchaguzi amewataka wagombea kutowagawa wananchi kwa misingi ya kidini ikiwa itatokea mgombea wa namna hiyo asichaguliwe bila kujali anatoka chama gani.
Aidha ameishukuru Serikali kuridhia kuwepo kwa kamati hii na kusema kuwa Serikali ikipata watu wanaompenda Mungu kazi inakuwa rahisi kwa kamati maana hata kiongozi akikosea anaweza kuonywa na kiongozi wake wa dini.
Ameelekeza viongozi wa kata kuunda kamati za amani ikiwa kutekeleza maagizo ya Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
"Waislam wanatakiwa kuwa na neno amani Kila wakati vinywani mwao hata wakristo Katika Zaburi 119 wameaswa kufanya hivyo kwahiyo amewataka watu wa dininzote kuitunza amani" Alisema
OCD KIGAMBONI JOHN IMORI
Kupitia kongamano la amani amesema pamoja na Polisi kuwa walinzi wa amani ya wananchi lakini ushirikiano kutoka makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini.
Jeshi la Polisi limekasimiwa kisheria kusimamia amani Katika kipindi Cha uchaguzi linasimamia amani na usalama kwa wagombea wa vyama vyote ili kuwagikia wananchi ambao ni wapiga kura .
Ilijeshi kulinda Mali na maisha ya watu ,usalama kwa wagombea ,watimiaji wanakuwa salama ,kuimarisha amani ,ulinzi kwa wahesbuji kura ,ulinzi Katika kusafiriha vyombo ama vifaa vya kupitia kura .
Kwa kipindi hiki pia Jeshi linatoa elimu kwa wananchi kujua wajibu wao wakati huu wa uchaguzi ,kuwajengea uwezo Jamii kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa dini ,boda boda na makundi mengine ya kijamii.
Pia linashawishi au kuhimiza kwa lengo la kufuatilia miendendo ya kichochezi , kutekeleza Sheria .
Baada ya Jeshi kutoa elimu hiyo wanakaidi kinachofuata ni kushurutishwa kwa wanaokaidi.
Amesema amani ndiyo msingi wa Maendeleo Jeshi linawataka wote kushiriki mchakato huu kwa kulinda amani lakini Jeshi halitasita kuchukua hatua kwa watakao leta ama kusababisha vurugu katika mchakato wa uchaguzi .
"Naomba viongozi wa dini mfanye Doria za kiroho wakati sisi tunafanya Doria za miguu na kuwakamata waharifu ninyi mnawahubiri wanaweza kuacha uovu na kuwa raia wema.
Charles Lawiso. Mwanasheria wa Wilaya Kigamboni
Amewataka viongozi wa dini kutoa elimu na hamasa kwa waumini wao kutoshiriki Katika uvunjifu wa amani,pia kuhamasisha wananchi /waumini kujitokeza kusikiliza mikutano ya wagombea na kushiriki zoezi la kupiga kura siku ya tarehe 28/oktoba.
Tume imeandaa mchakato wa uchaguzi kisheria ambapo inasheria mbalimbali na maadili ya uchaguzi ambayo Kila chama kimesaini kuyazingatia hayo.
Pia amewashauri wagombea ambao wamewekewa mapingamizi kutokuwa wasiwasi Kama wamekata rufaa maana time itayafanyia kazi na wasiporidhika wanaweza kwenda mahakamani.
Sheria za maadili zinamruhusu mtu ama mwanachama wa chama chochote kuhudhuria mkutano wa chama chochote bila kuzuiwa kwa kuwa kura itabakia kuwa Siri yake, katika zoezi la kupiga na kuhesabu kura zitawakilishwa na mawakala wake.
Post a Comment