MGOMBEA URAIS CCM AHUTUBIA MAELFU KIRUMBA MWANZA SOMA SERA NA AHADI ZAKE HAPA
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumatatu Septemba 7, 2020.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha kofia Msanii wa Bongo Flavor Nasib Abdul Diamond ambaye alikuwa akitumbuiza katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza kumsikiliza mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wagombea nafasi za Udiwani katika mkoa wa Mwanza wakisalimia kwa push-up na nyimbo za hamasa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mbele ya maelfu kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumatatu Septemba 7, 2020.
Sehemu ya umati wa maelfu kwa maelfu ya wananchi uliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumatatu Septemba 7, 2020.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya kuwahutubia Wananchi wa Mwanza katika Mikutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM leo tarehe 7 Septemba, 2020.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kabla ya kuanza kuhutubia.
Na Said Mwishehe, Mwanza
MWANZA wamefunika!Ndivyo ambavyo unaweza kuelezea kutokana na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli.
Akizungumza na wananchi hao wa Mwanza Dk.Magufuli amesema mapokezi ambayo ametapata ni makubwa sana na hajawahi kuyaona tangu aanze kampeni na wale ambao wanajipitisha pitisha wataisoma namba.
“Wananchi waliojaa hapa na walioko nje kinachofurahisha sio tu wana CCM bali ni wa vyama vyote, maana maendeleo hayana vyama, ahsante wana Mwanza na watanzania wote,”amesema.
Amewaambia wana Mwanza katika uchaguzi mkuu mwaka huu kama ilivyo kawaida yao hatamuangusha na yeye hatawangusha huku akikumbusha ahadi yake ya kuifanya Mwanza kuwa kituo kikuu cha biashara na wakati anatoa ahadi hiyo kuna mambo yalikuwa yanatakiwa kufanyika.
Dk.Magufuli ametaja mambo hayo ni kujenga miundombinu ya huduma mbalimbali na kuboresha huduma za ustawisha huduma za jamii na anafarijika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanya kazi pamoja na wananchi wa Mwanza.
Kuhusu barabara amesema katika Mkoa wa Mwanza miundombinu ya barabara imeboresha ikiwemo ya ujenzi wa barabara za lami akitolea mfano ya barabara ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilometa 17 kwa gharama Sh. bilioni Sh.20.1 na fedha zote zimetolewa na watanzania, lengo kuweka mkakati kupunguza msonagamano wa magari Jiji la Mwanza.
“Kwa Mwanza kumejengwa barabara nyingi, ikiwemo ya Mwanza, Nyakato hadi Busweli, Isamilo mji hadi Mji mwema, Pasiasi hadi Buzuruga kumepunguza msongamano.Tumejenga daraja la Furahisha kunusuru watu kupoteza maisha,”amesema Dk.Magufuli.
Ameongeza katika usafiri wa meli katika kipindi cha miaka mitano kuna mambo mengi yamefanyika kuboresha na kuimarisha usafiri wa meli na hivyo wamerakabati meli tano pamona kujengwa meli mpya mmoja kwa thamani ya Sh.bilioni 152.Wajenga vivuko.
Pia amefafanua bajeti ya mwaka huu wametenga Sh.bilioni 15 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa meli nyingine ikiwemo ya MV Umoja , pia ujenzi wa meli nyingine mpya ya kubeba mabehewa mengi zaidi ambao ni mpango inayokuja.
Kuhusu reli , amesema ujenzi wa reli ya ksasa ulishaanza kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na tayari wametangaza mkakati wa kuanza ujenzi wa reli hiyo kutoka Dodoma kuja Mwanza.
Huku akitumia nafasi hiyo kuomba wananchi kujiandaa kwa kupata ajira wakati ujenzi utakapoanza. Na ili reli hiyo ikamilike ndio maana tumekuja tena kuomba kura,”amesema Dk.Magufuli
Amefafanua kuimarisha kwa usafiri wa meli katika Ziwa Victoria umesaidia hata kwa wafanyabiashara kupata uwezo wa kiuchumi kuendelea na shughuli zao na kwamba hata bei ya bidhaa zinazosafirishwa kwa usafiri wa meli ziko chini.
Kwa upande wa usafiri wa anga, amesema Mwanza tayari wamejenga uwanja wa ndege ikiwa pamoja na upanuzi wa wa uwanja huo kutoka kilometa mbili 2.8 hadi kilometa 3.5, wameweka taa , kujenga rada, miundombinu ya kuhifadhi minofu, ujenzi wa jengo la abiria kwa uboreshaji huo ndege kubwa za mizigo zinatua Mwanza.
Hata hivyo amesema kwamba kuna watu ambao wamekuwa wakisema Dk.Magufuli ananunua ndege kama ndio zitampigia kura, madaraja eti ndio tayampigia kura , lakini amewajibu kuwa wanaotumia miundomboni iliyoyengwa na Watanzania ndio hao hao ambao watampigia kura.
Wakati akizunguza zaidi na maelfu hayo ya wananchi Dk.Magufuli amesema katika miaka mitano wameboresha upatikanaji wa huduma muhimu, ikiwemo afya, maji na umeme, wameboresha huduma za kibingwa.
”Wagonjwa wa moyo watapata huduma za matibabu hapa hapa, wenye magonjwa ya kansa nao watapata matibabu hapa hapa Mwanza, kujenga miunndombinu mengine ya afya yenye thamani ya Sh.bilioni bilioni 11.4.Pia tumejenga hospitali za Wilaya, vituo vya afya na zahanati,”amesema Dk.Magufuli.
Amefafanua katika miaka mitano wameletea magari 11 na boti moja kwa ajili ya kubebea wagonjwa,wakati kwenye elimu nako hakukuachwa nyuma na kwamba mengi yamefanyika na hilo limesaidia kuboresha elimu.
”Tumeongeza vyumba vya madarasa, mabweni, kufanya ukarabati wa shule konge, kukarabati Chuo cha Rutungulu na Sh.bilioni 53.7 zimetumika kutoa elimu bila malipo katika Mkoa wa Mwanza.
Kuhusu maji Dk.Magufuli amesema Sh.bililioni 92 zimetumika kubresha sekta ya maji na kwamba tayari zimetengwa Sh.bilioni 32 kwa ajili ya miradi mingine ya maji.
Dk.Magufuli amesema kuna mambo mengi ya maendeleo yamefanyika katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla na ndio maana amekuja tena kuomba kura za ndio katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Post a Comment