Maonyesho ya ubunifu wa mavazi kufanyika Desemba 4-6 Mwaka huu
Jukwaa la Maonyesho ya mavazi(Swahili Fashion week) limesema litaendelea na shughuli zake za kukuza vipaji vya wabunifu Nchini ili kusaidia kukuza sekta ya ajira kwa vijana kujiajiri wenyewe pasipo kutegeme utegemezi.
Akizungumza jijini Dar es salaaam Muasisi wa Jukwaa hilo ambaye pia ni mbunifu mkongwe wa mavazi Mustafa Hasaanali ambapo alisema wanawatoa hofu watu wote waliopo katoka sekta ya ubunifu na mitindo kuwa tamasha lililokuwa linasubiriwa linarajiwa kufanyika Desemba 4-6mwaka huu katika hoteli ya serena Dar es salaam.
Hassanal ameongeza kuwa maambukizi ya homa kali ya mapafu corona ilipoingia Nchini wabunifu wengi walipata hofu na tabu ya kuendesha shughuli zao kutokana sherehe mbalimbali kufungwa hivyo kukosa soko la kuuza bidhaa zao hivyo wanaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada zake za kukabiliana na gonjwa hilo.
"Tunashukuru Mungu kwa hali nzuri ya kiusalama kuhusiana na Janga la homa ya korona Nchini kwa sasa na kwa sababu hiyo maonyesho yamepangwa kufanyika na tayari tupo hatua za maandalizi"alisema Hassanali
Hata hivyo alisema mpaka sasa wabunifu Zaidi ya thelathini (30)kutoka ndani na nje ya Nchi tayari wamethibitisha ushiriki wao kwenye onyesho hilo mwaka huu wabunifu watakuwepo hadi wa nywele.
Kwa upande Mkurugenzi wa mauzo Hoteli ya serena ambao ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo mwaka huu ya Seraphin Lusala amesema uwepo wa shughuli kama hizo za matamasha makubwa ni uthitisho kuwa Tanzania imeweza kupambana na corona hivyokuendelea kuithibitishia Mataifa kuwa Tanzania ni salama.
\"Tunayofura kuwa furaha kuwa washirika wakuu Swahili fashion Week maonyesho haya tulipata matokea chanya katika maonyesho ya mwaka jana na hivyo tunataka kufanya kilicho bora zaidi mwaka huu"alisema Lusala
Lusala alisema kupitia sherehe na matamasha yanayoendelea Nchini yanaweza kutumika kama hamasa kwa Nchi jirani kufuaya nyayo za Tanzania
Aidha jukwaa hilo linawahasisha kwenye shindano la wabunifu chipukidhi maarufu kama Washington BenBella Emerging Designers Competition kwani tayari usajili umeshaanza washiriki wanaweza kujisajili kupitia kiunganishi kinachopatikana kwenye tovuti ya jukwaa hilo www.swahilifashioweek.com
Post a Comment