KMC FC YAICHAPA MBEYA CITY GOLI NNE BILA HURUMA
katika mchezo huo ambao ulikuwa na burudani ya aina yake, umetoa taswira kwa timu ya KMC FC katika kutimiza malengo ya kuweza kuchukua ubingwa katika msimu huu wa ligi kuu tanzania bara MWAKA 2020 hadi 2021.
mafanikio ya ushindi huo yametokana na uwezo ambao wachezaji wa KMC FC wameuonesha katika kipimdi cha dakika 90 za mchezo ikiwa ni pamoja na kuzingatia maelezo waliyokuwa wanapewa na mwalimu wakati wa maandalizi ya mchezo huo.
Magoli ya KMC FC yamefungwa na wachezaji Israel Mwenda, Hassan Kagunda, Abdul Hilary pamoja na Poul Peter na hivyo kuwawezesha mashabiki wa timu hiyo kuondoka uwanjani wakiwa na furasa na hivyo kutuma Salama kwa timu ya Tanzania Prison ambayo itakwenda kukutana nayo katika mchezo ujao.
Kikosi cha KMC FC leo kilikuwa na wachezaji ambao ni Rahim Sheik, Isra Mwenda, David Bryson,Lusajo Mwaikenda, Andrew Vicent, Hassan Kaparata, Hassan Kabunda, Kenny Ally , Poul Peter, Emmanuel Mvuyekule pamoja na Abdul Hillary.
imetolewa leo Septemba 7
na Christina Mwagala
Afisa Habari wa Timu ya KMC.
Post a Comment