Ads

DC MSAFIRI AITAKA KIGAMBONI KUILINDA AMANI NA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI.




Migogoro wa makaburi na msikiti baina ya mwekezaji  eneo la mwongozo umeisha kwa kushirikiana na kamati ya amani Kama alivyo agiza Mhe Rais Magufu baada ya kufanya ziara Katika Wilaya ya Kigamboni.

Ameyaema hayo mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara msafiri Katika kongamano la viongozi wa dini kuelekea ucgauzi mkuu na kuwataka wanakigamboni na viongozi wa dini kuitunza amani kwani ikipotea ni gharama kuipata

Kutokana na amani iliyopo majeshi yetu kwa Sasa yanafanya kazi ya kuendeleza  Maendeleo ambapo tusinge kuwa na amani tunge kuwa tuna utumia huo muda na gharama Katika kutafuta  amani .

"Unapopata kiongozi wa juu kuwa na maono tunapata umoja na mtangamano wa kitaifa Kama tulivyoona kiongozi wetu Raisi Magufuli akitetea rasilimali za taifa ,kujenga miundombinu ,hospitali na kuiondoa Corona  kwa kuwaelkeza watanzania wote kumuomba Mungu "Amesema DC msafiri.

Amesema Changamoto ambazo tumepitia zimetufanya kuwa wamoja Kama taifa  .

Hata hivyo amewataka wananchi wote kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi watakao iongoza Tanzania .

"Kuna msemo unasema  ukipenda ua penda na boga lake ,ukimchagua Magufuli chagua na wasidizi wake ,usichague boga tu ukakata majani yake utaishia hili Hilo hutapata lingine "Alisema

Aidha amewataka  wagombea waliowekewa pingamizi kufuata Sheria  na so kufanya vurugu au kuhujumu maendeleo

DC Msafiri  amasema  Rais Magufuli  kwa kuipenda Kigamboni ameitengea bilion  2.5  kwaajili ya kuimarisha hudu za umeme na Sasa kinajengwa kituo hapo Dege na unakamilika novemba  mwaka huu megawhats 54 pia  atajenga bara bara kilomita za  lami 121  na kwa Sasa bara bara  zimetengwa barabara 40 za kuanzia.

No comments