Ads

Clabu ya wananchi Yanga yazindua rasmi jezi mpya

 


Klabu ya Yanga , imezindua rasmi jezi zake mpya kwa ajili ya kuzitumia katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021, mbapo za Kijani zitatumika ugenini na njano nyumbani.


Jezi hizo zimeanza kuuzwa leo, kwa Tshs 35,000 katika Makao makuu ya Klabu hiyo kwenye Duka maalumu la Klabu na Maduka ya Wadhamini wao, GSM.

Katika uzinduzi huo ambapo Mjumbe wa kamati utendaji Yanga ambaye pia ni mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Eng Hersi Said ndiye aliyezindua huku wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wakishuhudia tukio hilo.

Mara baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba ambao ni wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga, amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua jezi halisi ili kuiongezea pato klabu hiyo.

No comments