Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Ummy mwalimu amepiga marufuku shule zote nchini kuwapa wasichana dawa aina ya Folic Acid na badala yake shule zimetakiwa kulima kuwajengea uwezo wa kulima maboga na mbogamboga katika bustani za shule.
Waziri Ummy amesema hayo leo wakati alipokua akihitimisha kilele cha Maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar Es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro ambayo yamefanyika mkoani Morogoro.
Waziri Ummy amesema ni marufuku kuwapa wanafunzi na wasichana balehe vidonge vya Folic Acid, badala yake fedha hizo zinazotolewa kwa ajili ya dawa hizo zitumike kuanzisha bustani shuleni ili kuzalisha vyakula vinavyotoa madini yanayopatikana kwenye vidonge hivyo.
“Mbali na kuanzishwa kwa bustani shuleni lakini pia fedha hizo zinaweza kupelekwa kwa vijana ili waanzishe miradi ya bustani za mboga kwa ajili ya kuzalisha mazao yanayozalisha asidi hiyo yakiwemo maboga, matunda na hata karoti badala ya kutoa vidonge kwa wanafunzi. Alisema
Post a Comment