UWT YAWATAKA WANAWAKE ILALA WASICHAFUANE WAKATI WA KAMPENI
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi akiongea na Wanawake wa Kata ya TABATA Wilaya ya Ilala katika ziara ya Viongozi wa UWT mkoa Dar es Salam leo Juni 30/2020 ( kulia) Mwenyekiti wa UWT Tabata Winnefrida Ndibalema(PICHA NA HERI SHAABAN)
NA HERI SHAABAN
UMOJA wa Wanawake UWT Dar es salaam imewataka Wanawake wa Wilaya ya Ilala wachukue fomu za uongozi kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani bila kuchafuana.
Hayo yalisemwa na Nuru Mwakivuma kutoka Umoja wa Wanawake Dar es Salaam, wakati wa ziara yake Kata ya TABATA halmashauri ya Ilala.
Nuru alisema wanawake wana uwezo mkubwa katika nafasi za uongozi hivyo wasirudi nyuma wakati wa kuchukua fomu za kugombea.
"Wanawake wakipewa madaraka ya uongozi nafasi yoyote ya uongozi wanaweza kuitumia hivyo tusirudi nyuma tutumie fursa hii Wanawake wa Tabata kuchukua fomu "alisema Nuru
Aidha Nuru aliwataka Wanawake wa TABATA halmashauri ya Ilala kutangaza kazi za utekelezaji wa Ilani zilizotekelezwa na Rais John Magufuli zikiwemo elimu bila malipo,ujenzi wa miradi ya kisasa Reli na barabara za kisasa na sekta ya afya vyote vilivyofanywa na Rais.
Alisema kabla uongozi wa Rais Magufuli wananchi walikuwa wakichangia fedha za jengo pamoja na ada ya ulinzi mara baada Magufuli kuingia madarakani ada zote zimefutwa.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi aliwataka Wanawake wa Wilaya ya Ilala kusemeana mazuri na kuunga mkono chama chetu kiweze kushinda kwa kishindo.
Amina Dodi alisema Wanawake wana mchango mkubwa kwa chama na serikali pia ni walinzi hivyo muda wa uchaguzi ukifika watumie fursa hiyo vizuri katika kugombea nyazifa za uongozi.
Aliwataka wanawake wa Tabata kumuunga mkono Rais Magufuli katika kukuza uchumi wa viwanda ili nchi yetu iweze kusonga mbele.
Post a Comment