SAUTI YA JAMII WAZINDUA KAMPENI YA ZUIA UKATILI KWA WANAWAKE
Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Selemani Bishagazi akitoa elimu siku ya kampeni ya kuzuia ukatili kwa Wanawake na Wasichana wa Jimbo la Ukonga (PICHA NA HERI SHAABAN)
NA HERI SHAABAN
SAUTI ya Jamii Kipunguni wamezindua Kampeni ya Kuzuia ukatili kwa wanawake na Wasichana na watoto Jimbo la Ukonga.
Akizungumza katika Kampeni hiyo ,Mkurugenzi wa SAUTI ya Jamii Kipunguni Selemani Bishagazi alisema lengo kuwapa mbinu za kupata kipato mbadala Wanawake na Vijana ambao vyanzo vyao vya kipato vimeathirika
" mafunzo haya ya kutoa elimu kwa wanawake na na wasichana kuzuia ukatili unaosababishwa na mlipuko wa COVID 19 corona kuzuia gharama ya vifaa kinga kwa kutumia maafisa Afya,maafisa ustawi wa Jamii, TAKUKURU, maafisa maendeleo ya Jamii, SIDO ,madawati ya Polisi na Wanasaikorojia "alisema Bishagazi.
Bishagazi alisema mradi huo unawalenga wana jamii hasa Wanawake na Wasichana, na watoto Kata za Kipunguni na Majohe, lengo kupunguza hofu ya unyanyapaa ndani ya Jamii, kutoa mbinu ya kujipatia kipato mbadala ili kuzuia ukatili unaosababishwa na umasikini wa kipato ikiwemo kupelekea Rushwa ya ngono .
Alisema kampeni hiyo inayowashirikisha maafisa mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii ikiwemo kutumia waandishi wa habari.
Aidha alisema shughuli za mradi wa Sauti ya Jamii Kipunguni zinafanyika kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa wa haki za wanawake na wasichana sambamba na mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo utengezaji wa Barakoa na vitakasa mikono.
Pia kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo uelewa wa haki za wanawake katika kupambana na athari za corona.
Post a Comment