TMB ,YATAJA UMUHIMU WA ULAJI NYAMA KWA BINADAMU
Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Dk. Imani Sichalwe, akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa.
BODI ya Nyama Tanzania (TMB) imewataka wananchi kula nyama bora na salama kwa kiwango kinachotakiwa ambacho ni wastani wa kilo 50 kwa mtu mmoja kila mwaka.
Hayo yamesemwa jana na Kaimu Msajili wa bodi ya nyama Tanzania, Dk. Imani Sichalwe wakati akizungumza na wandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa vilivyopo Temeke Jijini Dar es Salaam.
Sichazwe amesema ulaji wa nyama usaidia kuchochea homoni za mwili hivyo kila mtu anatakiwa kula nyama kilo 50 kwa mwaka ili kujenga afya bora na kupata protini kwa wingi mwilini.
Amesema, ulaji wa nyama ni muhimu katika mwili wa binadamu kwasababu usaidia kutengeneza mifupa, ujenzi wa akili pamoja na kuongeza homoni mwilini.
“Ulaji wa nyama unaokidhi viwango uisaidia jamii kujenga mwili na kuongeza homoni za kutosha na kuondoka na tatizo la magonjwa mbalimbali ikiwamo ukosefu wa uzazi,” amesema Dk. Sichwale.
Alisisitiza kuwa watu ambao awali nyama wamekuwa wakikosa vitu vingi katika mwili wao jambo ambalo uchangia kupungu kwa protini zao.
“Ubora wa protini ulioko katika nyama ni mkubwa zaidi kuliko ubora mwingine ambao unakosekana katika protini nyingine,”amesema Dk. Sichwale.
Akizungumzia Maonesho ya Sabasaba, Dkt. Sichwale amesema wamekuwa wakionesha kazi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na bodi hiyo ikiwemo kutoa mafunzo katika mmyololo mzima wa thamani ya nyama.
“Tukizungumzia suala la nyama linatakiwa lianzie katika mashamba ambako kuna uchaguzi wa mbegu, ulishaji mifungo pamoja na usafirishaji,” amesema Dkt. Sishwale.
Aidha amesema, wamekuwa wakiamasisha wananchi juu ya ujenzi wa Viwanda vya kisasa ikiwemo machinjio pamoja na kujua namna ya kusafirisha vyema mifungo na nyama.
Post a Comment