KATIBU WA BUNGE,AIMWAGIA SIFA VETA SABASABA
KATIBU Mkuu wa Bunge Stephen Kigaigai ameitaka Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), iongeza ubunifu na iwaimarishe zaidi vijana wanaopata mafunzo katika vyuo vyao hasa kwenye masuala ya ufundi na uendelezaji wa ubunifu wao.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba,mara baada ya kutembelea banda la mamlaka hiyo, Kigaigai amesema kiwa VETA imekuwa ikitoa mafunzo bora ambaye yanaendana sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya uchumi wa viwanda.
Aidha Kigaigai amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapaswa kuweka msisitizo kwa VETA katika kuhakikisha vijana wanaohitimu masomo yao wanafatiliwa na kutowapoteza katika ufundi wao.
Amesema pia kufanyike ufatiliaji wa kuangalia vijana wanapomaliza VETA wanaenda wapi na wanaendeleza vipaji vyao.
"VETA na Wizara ya Elimu wanatakiwa kushirikiana kuwafatilia vijana hawa wanapomaliza masomo yao hasa kuangalia wanapokwenda wapi na wanafanya nini," amesema na kuongeza
"Kama taifa itatumia elimu na wataalamu wanapatikana VETA nchi itafika mbali kwani mitahala ya mamlaka hiyo inaonyesha kuwa ni mizuri," amesema
Amesema VETA yenyewe ni kiwanda kwani wamekuwa wakizalisha Wataalam mbali mbali ambao wengi wao wanaajiliwa katika viwanda.
Post a Comment