TAWA YAZIDI KUWAVUTIA WATALII KUTEMBELEA MALIKALE ZA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA
Eneo la Kivutio la Magofu ya Songo Mnara
Bi.Mercy Mbogelah Meneja Mhifadhi malikale
katika Urithi wa utamaduni wa dunia magaofu ya Kilwa Kisiwani na Songo
mnara chini ya Mamlaka ya Usimamizi ya wanyamapori Tanzania TAWA
yaliyopo Wilayani Kilwa Mkoani LIndi akizungumzia vivutio vilivyopo
katika maeneo hayo.
Moja wa Msikiti uliopo Kilwa Kisiwani ukiwa katika ubora ni eneo moja wapo la kivutio kwa watalii
------------------------------ ------
JITIHADA
zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA
katika kutangaza malikale katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa dunia
Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara zinaendelea kuleta tija kwa
Mamlaka hiyo kutokana na wageni wengi kufika katika Hifadhi hiyo ili
kujionea vivutio hivyo.
Meneja Mhifadhi wa
maeneo hayo Bi. Mercy Mbogelah amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na
muitikio mzuri kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi baada ya serikali
kuruhusu shughuli za kitalii ambazo zilisimama kutokana na virusi vya
Corona
Akizungumza na wanahabari Bi Mbogelah ameeleza kuwa
vivutio hivyo vilivyo katika Mji wa Kilwa Mkoani Lindi vina historia ya
kipekee hapa nchini hasa ukizingatia kuwa ni Mji ambao ulikuwa ukitumia
sarafu yake.
Ameeleza kuwa mji huo ambao ulijizolea umaarufu
tangu karne ya 12 mpaka 16 ulikuwa ni kituo cha biashara ukanda wa Pwani
ya Afrika Mashariki na mataifa mbalimbali kama
Arabs,Indonesia,China,India na Ulaya ambapo walifika kufanya biashara na
masultan waliokuwa wanaishi kilwa.
Sanjari na
hayo Mji wa Kilwa ulikuwa chimbuko la utamaduni wa Lugha ya
Kiswahili,na Hivi leo kuna ushahidi wa majengo ya kale kama ngome ya
mreno misikiti ya kale visima vya kale N.K
Baadhi ya wageni
waliotembelea mali kale katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa dunia
magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania TAWA kutoka nje nchi wamesema kuwa wameridhishwa
na vivutio vilivyopo ndani ya eneo hilo na jitihada kubwa zinazofanywa
na TAWA za kuboresha miundo mbinu zinazoendelea ndani ya Hifadhi ya
Kilwa.
Mmoja wa wageni kutoka Nchini
aliyetembea eneo hilo ni Miss Utalii Mkoa wa Lindi 2020 Grace Mella
amesema kuwa ameamua kutembelea eneo hilo kutokana na historia ya
kipekee hapa nchini na yenye kusifika kwa kila pembe ya dunia.
Aidha
Miss Utalii Lindi ametoa wito hasa kwa jamii ya Kitanzania kuweza
kutembelea eneo hilo kwa lengo la kujifunza historia mbalimbali za
masultan katika Mji wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.
Post a Comment