Odama, Swahiliflix ni kama ndege wafananao kuruka kwa pamoja.
Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Odama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu aujio wake wa filamu iitwayo Mr.Kiongozi.
Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Jenifa Kyaka "Odama" amesema amekuja kivingine katika filamu yake mpya iitwayo "Mr.Kiongozi" .
Akizungumza na mwandishi wa habari jana Dar es Salaam katika uzinduzi wa filamu hiyo Odama alisema kuwa kampuni ya Aflix East Africa kupitia Swahiliflix app ndiyo wanaotambulisha ujio huo.
Alisema kazi juu ya utambulisho huo umefanya chini ya uandaaji wake kupitia kampuni yake mwenyewe iitwayo JFILM 4 LIFE.
"Ni raha sana kuona filamu za Kiswahili kupitia Swahiliflix kwa gharama nafuu , kuna vifurushi vya bei nafuu sana ," alisema Odama.
Kwa upande wake msemaji wa waanzilishi wa Swahiliflix Hosea Jemba alisema wamegundua kua watanzania wanapenda filamu zenye ubora wa hali ya juu jambo ambalo linawapa motisha kuhakikisha wanachapisha filamu zenye ubora wa hali ya juu ili kukuza soko lake.
Jemba ameeleza kuwa kuwepo kwa kampuni yao ya Swahiliflix kumetoa fursa kwa wasanii na wadau kuonesha kazi zao duniani kote huku lugha mama kiswahili ikiendelea kukua na kutangazwa dunia nzima.
Naye msanii mkongwe katika tasnia ya filamu nchini Hashi Kambi, alisema filamu hiyo itafanya mashabiki kupata burudani kubwa kwani ujembe wake umelenga jamii yote ya Afrika.
"Nimecheza kama kiongozi wa familia huku nikiwa kama baba mwenye familia huku watoto watoto wangu wakitumia jina langu vibaya kwenye jamii," alisema Hashim.
Kwa sasa wadau wanaweza kuona filamu za kiswahili kupitia Swahiflix kwa gharama za sh.3,000 kwa siku pamoja na sh.8,000 kwa wiki na sh.20,000 kwa mwezi.
Post a Comment