Ads

MKAKATI MKUBWA WAWEKWA KULETA MANUFAA ZAO LA MKONGE NCHINI.

ZAO LA MKONGE LAWEZA KUFUTA UMASIKINI - Mtanzania

Mwamba wa habari
Nitakribani  silimia nne  ya mazao ya mkonge  yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini, ambapo  asilimia 96  imekuwaikipotea kutokana na ukosefu wa nyenzo za kisasa za kutengeneza na kuzifanya bidhaa kuwa na kiwango kinachokidhi ubora.

Hayo yameelezwa  katika mkutano wa Ana kwa Ana (B2B)wa wafanyabiashara kwenye Maonesho ya 44,ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), Afisa Mipango na Utafiti wa TSB,Frederick Sospeter alisema zao la mkonge lina faida nyingi lakini bado mazao hayajatumika ipasavyo.

"Zao la  mkonge na bidhaa zake  lina faida nyingi na linatumika kwenye sekta mbalimbali kama vile viwanda,kilimo, viwanda vya kutengeneza dawa ,kwenye meli,ndege na magari ambapo nyuzi za mkonge hutumika na bidhaa nyingine  ya zao hilo hutumika kama chakula cha mifugo na mbolea,ila hapa nchi  bado hatuna teknolojia inayochochea matumizi mkonge''

Changamoto  ya teknolojia duni imeifanya bodi hiyo kufikiria zaidi na kuweka lengo lengo na  kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wanazalisha tani 120,000 za zao la mkonge   tofauti na sasa  ambapo zao hilo linazalisha kiasi cha tani 40,000 kiasi ambacho ni kidogo.

Alifafanua kuwa,  moja ya hatua walizofanya kuhakikisha wanapata wawekezaji hukujuhudi juhudi zikiendelea za kuwapata wawekezaji ili kuwekeza kwenye zao hilo na kuwa na teknolojia ya viwanda vitakavyotumika kuchakata mazao hayo kupata bidhaa mbalimbali zenye ubora na kupata fedha nyingi kuliko kuendelea kuzalisha malighafi ambayo haina thamani kubwa zaidi

Akitoa mchango wa mawazo  katika  mkutano huo wa uliowashirikisha wadau mbalimbali wa masoko wakiwemo Soko la Mazao Tanzania (TMX) alisema kuanzia Desemba mwaka huu wataanza kuuza mazao ya mkonge ya wakulima wadogo kama njia mojawapo ya kuinua sekta hiyo.

Taarifa ya  TMX  inasema , wanazungumza na bodi ya vyama vya msingi vya mazao (AMCOS),ili kukamilisha baadhi ya taratibu ili ifokapo Desemba mwaka huu waanze kuuza mazao ya mkonge ya wakulima wadogo kwa mfumo wa kieletroniki.

" Mwishoni mwa mwaka huu tutaanza  kuuza mazao ya mkonge ya wakulima wadogo wa zao hilo tutayaweka kwenye soko letu ambalo ni la wazi ili yapate wateja,"alisema  Augustino Mbulumi, Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa TMX.

No comments