Ads

Avis Legal yawakutanisha wanafunzi viongozi vyuo mbalimbali

Asasi  hisiyokuwa ya kiserili Avis legal wiki iliyopita ilifanikiwa kuandaa kongamano la vijana  na kuwakutanisha vijana mbali mbali wenye levo za uongozi katika vyo mbali mbali nchi.
Kongamano hilo limeeleza kuwa vijana ni kundi kubwa katika nchi na kua hawawezi kutenganishwa katika nyanja mbali mbali.
Akizungumza kwenye kongamano hilo Wakili Hamza Jabir kutoka Avis legal alisema wanaisapoti serikali katika kuingia uchumi wa kati na kuelekea uchumi wa viwanda.
"Ofisi ya wakili ya Avis legal kwa kushirikiana na serikali na wananchi imefanikiwa kufanya kazi mbalimbali ," alisema Hamza.
Kwa upande wake wakili Henry H.Mwinuka kutoka asasai hiyo alisema vijana ni lazima waelewe nafasi yao na kuwa kongamano hilo limewatia moyo wa kuweza kuandaa kakongamano mengine.
"Vijana wawe na mtazamo wa kujiamini hali hiyo itachangia kufanya maendeleo binafsi na taiga," alisema Mwinuka.
Alisisitiza vijana kuwa na magenda za maendeleo na kua cha tabia ya kuchukua rushwa.
Naye Betty Tibasima Jeremiah ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa  serikali ya wanafunzi kutoka Raid (DIT) alisema katika mafunzo vijana na uongozi ameweza kujifunza kujiamini na kwa kuchukua atua binafsi na kwa taifa katika kufanya maendeleo.
Katika kujipambanua zaidi   mwaka 2019 ofisi ya wakili ya Avis legal kwa kushirikiana na serikali na wananchi imefanikiwa kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kampeni ya kuzuia mifuko ya plastic na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili kijinsia na watoto.

 Avis legal wanajukumu la kuisaidia jamii na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanatatua baadhi ya changamoto zilizopo.
Avis legal kwa mwaka 2019 ilifanikiwa kuzindua kampeni ya ukatili wa kijinsia na watoto kwa Tanzania bara na visiwani ikiwa na kauli mbiu ya “usikubali kuwa moja wao usikae kimya” ikiwa na maana kuwa tukio linapotokea jamii isikae kimya kwani kukaa kimya pia ni mojawapo ya ukatili.
Mbali na hayo Ofisi ya Avis legal imeweza kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya watanzania kupitia njia mbalimbali ikiwa ni mojawapo ya njia ya ofisi ya kutoa gawio kwa jamii inayowazunguka.

No comments