Ads

RC MAKONDA AKABIDHI MSAADA WA GARI, VITANDA, MAGODORO NA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 467.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 12 amekabidhi msaada wa Gari moja, Vitanda 600, Magodoro 600 na Mashine za kupumulia 7 kwa Manispaa ya Ilala na Kigamboni kwaajili ya kutoa huduma kwenye Hospital mpya za Wilaya hizo.

Katika Mgawanyo wa vifaa hivyo alivyokabidhi RC Makonda, Wilaya ya Kigamboni imepatiwa Gari Moja, Mashine 5 za kupumulia (oxygen concentrator), Vitanda 300 na Magodoro 300 ambapo kwa upande wa Ilala wamepatiwa Magodoro 300, Vitanda 300 na Mashine 2 za kusaidia Wagonjwa  kupumula.

RC Makonda amesema mbali na kukabidhi vifaa hivyo tayari Serikali imeingiza kiasi cha shilingi milioni 300 kwa kila Wilaya kwaajili ya Kukamilisha miundombinu ya mawasiliani kwa Majengo ya OPD, Mahabara, Majengo ya upasuaji na Majengo ya Mahabara kwa lengo la kurahisisha huduma.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi kwenda kupata huduma za Afya kwenye Hospital Mpya za Wilaya ya Kigamboni na Ilala kwakuwa tayari zimeanza kutoa huduma tokea Juni Mosi mwaka huu.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka watumishi wote wa Afya waliohamishiwa kwenye Hospital mpya za Wilaya kuhakikisha wanafika na sehemu zao za kazi.

RC Makonda pia amesema kuwa amefanikiwa kupata wadau wa Taasisi ya Doris Molel Foundation ambao wameahidi kumpatia vifaa kwaajili ya watoto njiti na muda wowote kuanzia sasa vitakabidhiwa kwa Hospital ya Wilaya ya Kigamboni.


No comments