MWEKEZAJI AJITOSA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI WADOGO, ATANGAZA MIKOPO ISIYO NA RIBA, ATOA MAGARI, NYUMBA, VIWANJA.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) Bw. Ussi Said Suleman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
wadogo wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na kuwekeza katika Kampuni ya
Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) ambayo inatoa mikopo ya aina
mbalimbali isiyo na riba pamoja kutoa faida kila mwezi.
Kampuni ya Uwekezaji
ya Online Small Capital Mobile (OSC) imelenga kuwasaidia na kukuza mitaji ya
wafanyabiashara wadogo, kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuhakikisha wanapiga
hatua katika nyanja za kiuchumi.
Akizungumza na
waandishi wa habari wiki hii jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya
Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) Bw. Ussi Said Suleman, amesema
kuwa lengo ni kuunga mkono Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar katika
kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanafanikiwa.
Bw. Suleman
amesema kuwa baada ya mfanyabiashara mdogo kujiunga
na kuwekeza kuanzia sh. 50,000 atapata fursa ya kukopeshwa kulingana na uwitaji
wake ikiwemo mtaji, kiwanja, nyumba, bajaji, friji, magari ili kuhakikisha
anapiga hatua kimaendeleo.
“Mtu yoyote
anaweza kujiunga na Kampuni yetu kwa kufika ofisini kwetu Zanzibar au kujiunga kwa
kutembelea mtandao wetu wa Online Small Capital Mobile au kupiga simu ya kiganjani
kupita namba 0718 12 55 77, 0776 423 639”amesema Bw. Suleman.
Bw. Suleman
amefafanua kuwa ili mtu aweze kujiunga anatakiwa kuchukua fomu kwa gharama
ndogo ya sh.10, 000 ambayo itamuwezesha kujiunga na kuanza mpango wa kufikia
ndoto zake kibiashara.
“Ni fursa kubwa
kwa watu wenye kipato cha chini, lengo letu ni kuwasaidia ili kutimiza ndoto
zao, tunafanya hivyo kutokana tunajua wengi hawana mitaji ya kuanzisha biashara,
lakini wakijunga na kampuni wanapata uwezo kukopa na kupiga hatua za kiuchumi”
amesema Bw. Suleman.
Ameeleza
kuwa mpaka sasa watu 1,500 wamechangamkia fursa kwa kujiunga na Kampuni ya
Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC), huku 500 wemeshapatiwa mikopo
ambayo ina mifumo rafiki ya kuwalipia madeni kupitia faida yao ya kila mwezi.
Amesema
lengo ni kuwafikia wanachama zaidi ya 5,000 wenye kipato cha chini ili waweze
kuwasaidia kupitia ubunifu wa kuwekeza kupitia simu ya kiganjani.
Bw. Suleman
ametoa wito kwa serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwa na utaratibu wa
kutoa ruzuku kwa makampuni yanayofanya vizuri ili ziendelee kusaidia jamii
katika nyanja mbalimbali katika jamii.
Kampuni ya
Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) imeanzishwa mwaka 2019 Zanzibar ambayo
imelenga zaidi kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili waweze kupiga hatua
kiuchumi kwa kuwakopesha mikopo isiyo na riba baada ya kujiunga.
Kampuni ya
Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) inatoa mikopo ya mbalimbali
ikiwemo magari na nyumba pamoja kutoa ushauri wa kibiashara.
Post a Comment