Ads

MD KIGAMBONI AWATAKA WANANCHI KUFUATA SHERIA YA MATUMIZI YA ARDHI



Na John Luhende
Halmashauri ya  Manispaa ya Kigamboni imewataka wananchi wanaotaka kubadilisha matumizi ya ardhi kati viwanja vyao kufuata utaratibu uliowekwa na serikali ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza .

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ng'wilabuzu Ludigija  wakatika kikao cha baraza la Madiwani kiliket leo kupokea na kujadili  taarifa za utendaji kutoka katika kata zote tisa za Manispaa hiyo ambapo  kubadilisha matumizi ya maeneo bila taarifa ni kosa kisheria.

Aidha  Ludigija ameeleza utaratibu wa kufuata kabla ya kubadilisha matumizi ya ardhi kuwa mhusika anapaswa  kuandika barua kwenda ofisi ya Mkurugenzi ataelekezwa kuweka tangazo la wazi ili kama kuta kuwa na pingamizi liweze kufanyiwa kazi kabla ya maamuzi.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo Maabda Suleiman Hoja amewakaribisha wawekezaji kuwekeza kigamboni kwani bado kuna ardhi ya kutosha .

''Katika Manispaa za Dar es salaam ,ni Kigamboni pekee ambayo bado inaeneo la kutosha kwa uwekezaji  naomba wawekezaji waje "Alisema.

Naye Naibu Meya wa Manispaa amepongeza ushirikiano wa Madiwani na Mkurugenzi kwani umesaidia kuleta maendeleo kwa wananchi.

No comments