Ads

Kumekucha CCM, JPM achukua fomu kuwania Urais

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli, leo amechukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama chake kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Rais Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally kwenye Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.
Zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi upande wa Tanzania Bara na Zanzibar limeanza tarehe 15 mwezi huu na litakamilika tarehe 30 mwezi huu.

No comments