Ads

Jacline Mengi :Ahamasisha Kuwasaidia Wenye Maitaji Maalum.


Taasisi za kiserikali zisizo za kiserikali pamoja na mtu mmojamoja kwa jinsi Mungu alivyowabariki kuwa na desturi ya kutoa na kuwasaidia wenye mahitaji kwani kufanya hivyo ni kuongeza baraka katika familia zao.
Ushauri huo umetolewa na Mlezi wa Taasisis iliasisiwa na Marehem Regnal Mengi JAKLINE MENGI katika kukabidhi msaada wa Mafuta ya ngozi na kofia kwa chama cha watu wenye ualbino  ambao hawana uwezo wa kununua vifaa hivyo ambavyo ni msaada wa kujikinga na mionzi ya jua.

Hata hivyo amesema Mara baada ya kukabidhi msaada huo kiongozi mkuu wa Taasisi hiyo bi Jackline Mengi.

"Nashukuru kwa mwaliko nilioupata ila  naomba Serikali nayo isaidie sababu mimi sitaweza peke yangu " alisema.

Aliongeza  kusema kuwa ushirikiano na watu binafsi utasaidia sana kwa jamii hivyo ya watu wenye ualbino hivyo  kuwa kutoa ni moyo basi watu wajitoe kwa wengine.

Ikumbukwe kuwa Baraza kuu la umoja wa Mataifa kunako tarehe 18 Desember 2014 ilitangaza kwamba kuanzia juni 13 2015 jumuiya ya Kimataifa ilipanga kuwainaadhimisha siku hiyo ya Kimataifa.

Siku hiyo  ya kimataifa ya kupambana na unyanyapaa dhidi ya walemavu wa ngozi Albino tangu wakati huo jumuiya ya Kimataifa inaweza kuwasilisha katika utofauti ili kuhakikisha kunakuwepo na ushirikishwaji wao kwakuwasikiliza changamoto Zao na kuzipatia ufumbuzi.

No comments