Ads

GSM YAELEKEZA NGUVU KUIFANYA YANGA KUWA KABLU KUBWA BARANI AFRIKA.

Kabla ya Yanga Afrikans kupitia mdhamini wake Kampuni ya GSM  imesema kuwa inaendelea na harakati za kuifanya  timu kuwa tishio Barani Afrika kwa kuwekeza kwa  wanachama.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM Hersi Said, alisema timu ya Yanga ina mashabiki na wanachama  wengi nchi nzima ambao wakitumika vizuri wanaongezea mapato kupitia ada ya wanachama.

Alisema kuwa wanachama hao  wanaweza kusaidia timu kwa  kujenga uwanja wa mazoezi pamoja na ununuzi usafiri aina ya bus kitu ambacho kitasaidia kuongeza uwezo wa viwango vya wachezaji katika timu hiyo.

"GSM watawafanya mashabiki, wanachama kuwa wamiliki wa klabu na kwamba anaimani mfumo huo ambao utaondoa changamoto ndani ya klabu ya tyanga katika kuwalipa mishahara wachezaji, makocha pamoja na safari za mechi " alisema Hersi.

Alisema kuwa uwekezaji wa kuweka fedha kwenye timu sio sahihi katika vilabu vyetu hapa nchini , kwani havina mapato ya kutosha kutokana kila mwaka vinapata hasara ya mapato.

Pia alitolea mfano kwa kusema kuwa wanachama na mashabiki wakiwa tu 500,000 wataweza kuchangia ada ya Sh 1200 kwa mwezi au mwaka klabu hiyo itapata Shilingi Bilioni 6 zitakazo weza kutumika kujenga viwanja  vya mazoezi pamoja na kununua usafiri.

Alifafanua kuwa uwekezaji kupitia wanachama ni kitu kizuri jambo ambalo litasaidia timu hiyo kusonga mbele kimaendeleo na kuwa timu ya mfano barani afrika.

"Timu itakuwa na uwezo wa kushindana na vilabu vikubwa Afrika vikiwemo TP Mazembe na vingine ikiwemo kutoka nchini Misri " alisema.

Hata hivyo ameeleza kuwa mpaka sasa tayari wameweza kumleta kocha wa viungo kutoka Afrika Kusini pamoja na kuwasainisha wachezaji watano.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika vipindi vyote vya mabadiliko hayakufanikiwa kutokana na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kukosa elimu sahihi ya mabadiliko yanayoitajika kufanyika hali iliyochangia klabu kuyumba kiuchumi.

Katika hatua nyengine amebainisha kuwa tayari ameweza kuingia mkataba na kampuni inayo endesha Ligi Kuu ya Hispania La Liga chini ya udhamini wa kampuni ya GSM kwa ajili ya kuhakikisha mipango yote inakwenda sawa.

Alisema kuwa thamani ya mkataba huo iliyoingia kablu ya Yanga chini ya udhamini wa kampuni GSM ni shilingi bil 2.6 katika kipindi cha miaka mitatu.

Mwandisi Hersi anasisitiza kuwa wakati wanajangwani  hao wakielekea kwenye mchakato wa mabadiliko GSM wamejipanga kuwekeza kwenye mtaji wa mashabiki ambapo kwa wingi wa wanachama na mashabiki wanaimani watafanya klabu hiyo kuwa imara.

No comments