GSM Yatoa Kitita cha Mil 30 kwa Wachezaji Yanga kuikalisha Kagera Suger FA.
MKURUGENZI wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM Eng.Hersi Said amesema nia yao kuu ni kufanya furaha kwa wanajangwani kwa kukabizi timu hiyo kwa wananchi katika mfumo wenye manufaa .
GSM inayomilikiwa na mfanyabiashara bilionea Gharib Said Mohamed, ambaye ni rais wa makampuni ya GSM ndiye muwezeshaji
aliye na nia hiyo muda huu ametoa Mil 30 ilikuchangia kupata matokeo katika mechi yao dhidi ya Gagera Suger inayochezwa leo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi muda huu amesema benchi la ufundi na wachezaji wrote tumetoa pesa hizo sasahivi kuhakikisha tunaibuka na ushindi.
Matokeo ya awali katika mchezo wa Ligi Kuu yanaipa Kagera wasiwasi kuwa yatauchochea mchezo wa leo kuwa mgumu katika robo fainali ya kombe la shirikisho la Azam kwenye uwanja wa Taifa.
Alisema wao kama wawekezaji wanataka kuonesha ukubwa wa mipango yao kuibadili Yanga SC na kurejesha utemi wake nchini na nje ya nchi lakini kwa sasa wanafanya kwa mapenzi yao ya dhati kwa timu ya wananchi.
"Yanga ina mashabiki na wanachama wengi nchi nzima ambao wakitumika vizuri wanaongezea mapato kupitia ada ya wanachama," alisema Eng.Hersi.
Sasa tuna sisi tiza kueleweka kwa kauli yetu mapato yanaweza kusaidia kujenga uwanja wa mazoezi na mechi na pia ununuzi wa basi na upande wa wachezaji kununuliwa wenye viwango vya juu.
"Tunataka wanachama na mashabiki , kuwa wamiliki wa klabu na kwamba na kuamini mfumo huo wa utaondoa changamoto timu katika kuwalipa mishahara wachezaji, na makocha pamoja na safari za mechi " alisema Hersi.
Alisema uwekezaji wa kuweka hela kwenye timu sio sahihi katika vilabu vyetu nchini , kwani havina mapato ya kutosha katika kila mwaka vinapata hasara ya mapato na hali hiyo ilishafanywa na wadhaminiwengine waliopita na kuacha changamoto zikiwa zile zile za hasara.
"Naweza kutolea mfano kuwa kupata Bilioni 6 tu , kwa baadhi ya wanachama hai 500,000 kwa ada za mwezi inawezekana na kufuta kabisa taswira ya kujiendesha kwa hasara," alisema .
Wanachama na wakiwa tu 500,000 wataweza kuchangia ada ya Sh 1200 kwa mwezi au mwaka klabu hiyo itapata Shilingi Bilioni 6 zitakazo weza kutumika kujenga Uwanja ,viwanja viwili vya mazoezi ,ununuzi wa basi .
Yanga yenye maskani yake mitaa ya jangwani Kariakoo itakuwa na uwezo wa kushindana na vilabu vikubwa Afrika .
Kwa upande wao kama wadhamini kwa sasa tayari wameweza kumleta kocha wa viungo kutoka Afrika Kusini pamoja na kuwasainisha wachezaji watano .
Alipambanua kuwa mbali na hilo imepitia vipindi tofauti katika kufanya mabadiliko kama yale wakati wa mdhamini Yusufu Manji akiwa Mwenyekiti wa Yanga .
Mkurugenzi huyo wa uwekezaji alisema kuwa katika vipindi vyote hivyo mabadiliko hayakufanikiwa kuyokana na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kukosa elimu sahihi ya mabadiliko yanayo itaka kufanyika hali iliyochangia kuyumba kwa uendeshaji kiuchumi.
Alieleza kuwa kuyumba kwa uchumi kulikotokea ikiwemo changamoto ya mishahara ya wachezaji na makocha ambapo katika kuhakikisha mabadiliko yanafanikiwa timu imeweza kuingia mkataba wa huduma ya ushauri.
Tayari imeweza kuingia mkataba na kampuni inayo endesha Ligi Kuu ya Hispania La Liga chini ya udhamini wa kampuni ya GSM.
Aliweka wazi kuwa thamani ya mkataba huo iliyoingia Yanga chini ya udhamini wa kampuni hiyo ni shilingi bil 2.6 katika kipindi cha miaka mitatu.
Post a Comment