Ads

BAADA YA KULAZIMISHWA SARE NA JKT ,YANGA YATOA ADHABU KALI KWA LAMINE



Na Zainab Nyamka.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umefikia hatua ya kumkata mshahara beki wake wa kutumaniwa baada ya kuonesha mchezo usio wa kiungwana kwa mwenzake.

Yanga ilicheza mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania na kumalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Lamine Moro sambamba na Mwinyi Kazimoto walioneshwa kadi nyekundu dakika za lala salama katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa sana.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kocha wake pia umeomba radhi kwa wanachama wa Yanga na wapenda mchezo wa mpira wa miguu kwa kitendo kilichooneshwa na beki huyo wa kimataifa ambapo ameeleza kuwa ni mara ya kwanza kulionesha.

Naye Lamine amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa soka kwa kitendo alichokifanya ambacho si cha kiungwana .Katika mchezo huo, JKT Tanzania walikuwa wa kwanza kuandika goli la kuongoza kupitia kwa Mchezaji wake Michael Aidan katika dakika ya 36.

Hadi mapumziko, JKT walikuwa wakiongoza kwa 1-0 .

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kusaka goli la kusawazisha kupitia kwa Mshambuliaji wake Patrick Sibomana akimalizia mpira uliotemwa na golikipa baada ya kupangua shuti la Haruna Niyonzima.

Hadi dakika 90 zinamalizika, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Yanga akifikisha alama 55 akisalia nafasi ya tatu nyuma ya Vinara Simba na  wa pili akifuatiwa na Azam Fc.

No comments