WAZAZI TUNGI WAHOFIA WATOTOWAO KUIGA TABIA ZA MADADA POA.
Mwamba wa habari
Wananchi wanaoishi maeneo ya kata ya Tungi Manispaa ya Kigamboni wameiomba serikali kuwanusuru watoto wao ili wasiige tabia chafu zinazo endelea katika eneo hilo ambapo madada poa wamehamia eneo hilo.
Wanachi hao wakizungumza na Mwamba wa habari ,wamesema wameshangazwa na mkazi mwenzao (..) kwa kuwakaribisha kuendesha shughuli hizo haramu ili hali akijua kuwa kuna Watoto na wana weza kuathiriwa na hali hiyo.
"Ndugu Mwandishi kama unavyoona hapa tuna Watoto wakike na wakiume hapa wanajifunza nini ? tunaomba fikisha kiliochetu kwa Serikali watuondolee hawa watu "Alisema mmoja wa wakazi hao.
Kwa upande wa akinamama baadhi yao wamelalamikia hali hiyo kuwepo eneo lao kwani hata waume zao wamkuwa na tabia za kwenda kupata huduma kwa madadapoa na baadhi yao hata hela ya matumizi nyumbani hawaachi wamekuwa wakizitumia kununua ngono .
"Mume wangu hata hanijali nina Watoto watatu hatoi hela ya matumizi mpaka mimi nikahangaike ndipo tule lakini siyo kwamba hana hata kidogo amekuwa na tabia ya kwenda katika hiyo nyumba pesa zote wana mmaliza kwakweli viongozi wa serikali waliangalie hili suala nikero kwetu"Alisema (...) kwa uchungu.
Mwamba wa habari, imemtafuta mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama ya mtaa huo pamoja na Diwani wa katahiyo Ernest Mafimbo nakukiri kupokea malalamiko ya wananchi hao na kwamba wanaendelea kulifanyia kazi.
"Nimefika eneo hilo nikamkuta kijana mmoja wa kiamasi analinda na nimemwita mmiliki wa nyumba hiyo nikamuuliza amenionesha vibali vya nyumba ya kulala wageni (Guest house) kutoka manispaa ya Kigamboni lakini cha kushangaza hakuna viongozi wa ngazi za chini waliohusishwa hata vigezo hivijafikiwa nyumba yenyewe hata kuna vyumba viwilitu vyenye milango vile vingine havina hata milango" Alisema Mafimbo.
Pamoja na hayo diwani huyo ameseme alipeleka taarifa hizo katika vyombo vya dolla na polisi walifika eneo hilo na hali ilitulia na ameshangazwa na kuibuka upya kwa hali hiyo na kusema kuwa Wilaya isha wahi kuchukua hatua kazi za kuvujna na kutaifisha eneo fula katika kata kigamboni ambalo lilikuwa linaendesha biashara ya ukahaba.
Post a Comment