Ads

DIWANI MJEMWEMA :KWAKIPINDI KIFUPI NIMETEKELEZA AHADI ZANGU NAISHUKURU SANA CCM.



Mamwa wa habari
Diwani wa kata ya Mjimwema Selestine Maufi  amewashukuru wananchi wa kata ya Mjimwema  kwa mwitikio mkubwa  katika kuchukua mikopo inayotolewa na halmashauri kwaajili ya akinamama Vijana na Walemavu .

Diwani huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Mwamba wa habari  utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo amesema alifanya kazi kubwa katika kuwahamasisha wananchi ili kuchukua mikopo hiyo isiyokuwa na riba ili iweze kuwainua kiuchumi katika kuendeleza biashara zao.
"Nawashukuru sana hawakuniangusha  katika kata za Manispaa ya Kigamboni hapa Mjimwema ndiyo imeongoza kwa vikundi vingi kuchukua mkopo hii ni kwasababu mimi Diwani wao nilihamasisha vyakutosha  nafahamu hali kwa sasa imekuwangumu sana kibiashara katika kipindi hiki cha COVID 19 lakini nawaomba sana tujitahidi kurejesha  mikopo hii ili  nawenzetu wengine ambao hawajapata waweze kupata"Alisema

Aidha akizungumzia ahadi alizotoa kwa wananchi wakati anagombea  amesema amesema ametekeleza kwa asilimia kubwa nakwamba zimeendelea kutekelezwa kutokana upatikanaji wa fedha .

"Moja ya ahadi zingine ni kuhusu barabara za ndani  pamoja na kwamba hizi barabara za ziko chini  ya TARURA  lakini mimi kama Diwani zinanihusu nimekuwa nikichukua malalamiko ya wananchi na kupeleka TARURA  tulitegema kujenga barabara nyingi lakini kwa sasa tunajenga barabara moja  ile ya Mjimwema kisota mpaka soko maziwa"Alisema

Aidha amesema katika barabara zingine ambazo zimeharibiwa na mvua  wanajipanga kuzichonga na  kujaza vifusi ilikuondoa usumbufu kwa wananchi wanaotumia maeneo hayo.
Hata hiyo amekishukuru Chama Cha Mapinduzi  kwa kupokea vizuri akitokea upinzani na kusema kabla kuingia chama hicho alipatachangamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu ya udiwani hali iliyopelekea kuchelewa kwa baadhi ya shughuli za maendeleo.

"Uongozi wa CCM kuanzia ngazi ya tawi kata ,wilaya , mkoa paka taifa ,napenda niwashukuru sana walinipokea na nimeona tofauti pale mwanzo na sasa tunaweza kupanga jambo likatekelezeka  kwakuwa naweza kuongea vizuri na Mkurugenzi ,Mkuu wa Wilaya  katibu tawala na viongozi wengine kwa muda mfupi nimefanya mambo makubwa ambayo  mwanzo sikuweza kuyatekeleza  "Alisema

Nao baadhi ya wananchi wanaotumia barabara ya Maweni mjimwema kisota mapaka soko maziwa wamemshukuru Diwani wao kwa kutoa msukumo mkubwa katika ujenzi wa barabara hiyo kwani imesaidia kuondokana na adha waliyo kuwa wanaipata  na wameomba wajenzi waweze kuimalizia baada ya kipindi hiki cha mvua .

"Tuna shukuru sana barabara hii inaenda kukamilika tena kwa kiwango cha lami ila tunamuomba diwani asichoke kutupigania sisi wananchi wake aende aongee na mamlaka husika tunataka daladala zianze kupita hiinjia ili kurahisisha usafiri na biashara zetu hapa zipate kuchangammka"  Alisema Winnifrida Kimario.

No comments