Ads

WAMILIKI WA VIWANDA NCHINI WAELEKEZWA KUKATA BIMA ZA MOTO


Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda nchini
kuhakikisha wanakata bima za moto ili pale
wanapokumbwa na ajali za moto wapate wepesi wa
kulipwa fidia za mali zao.



Bashungwa alitoa wito huo akiwa ziarani Karagwe
mkoani Kagera 17 mei 2020, baada ya kutembelea na
kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir
AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020
nakuona mashine zilivyoharibika baada ya kuunguzwa
na moto ambao chanzo chake ni hitilafu ya umeme
iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua
kubwa iliyonyesha siku hiyo.



Akiongea baada ya kukagua Mhe. Bashungwa alitoa
pole kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho Karim Amri
pamoja na wafanyakazi ambao kwasasa wamepoteza
ajira zao, ambapo alirithishwa na hatua ambazo
zimekwishachukuliwa na wamiliki wa kiwanda hicho
ambazo ni kufatilia bima kwaajili ya kulipwa fidia.



“Tunapokuwa na viwanda hatujui mambo ya kesho
na keshokutwa, mambo ya ajari unaweza kupanga
kila kitu lakini hakuna anayetegemea ajari itatokea muda gani, kwahiyo kupitia kiwanda hiki nitoe wito
kwa viwanda vyote nchini tuwe tunakata bima, maana
kiwanda hiki kimeungua lakini walikuwa na bima ya
moto.”



Awali meneja wa kiwanda hicho Daniel Ndayanse
akitoa taarifa kwa Waziri alieleza hasara walioipata
baada ya kufanya tathimini ya hasara iliyotokana na
kuungua kwa kiwanda hicho kuwa ni mashine za
kiwanda ni takribani Tsh.1,328,940,000.00 na jingo la
takribani Tsh. 49,275,750.00 na kuongeza kuwa
kiwanda kilikuwa na waajiliwa wa kudumu 16 ambao
wapo kwa kipindi chote cha mwaka na wakati wa
msimu huwa kinaajili watu kuanzia 800 hadi 1000
kulingana na kazi ya siku.



Aidha, Meneja alieleza kuwa “Kiwanda chetu tulikuwa
tumekiimalisha kwa kukifanya cha kisasa ambapo
tuliweza kuzalisha kati ya tani 50 hadi tani 65 za
kahawa safi ambazo ni takribani gunia kati ya 800
hadi 1,000 kwa masaa 24, kwa kukoboa kahawa
maganda kati ya tani 115 hadi tani 140 kwa masaa
hayo 24 kama hakuna tatizo la umeme.”



Kwaupande wake mmiliki wa kiwanda Bw.Karim Amri
alimshukuru Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa
kuendelea kuimarisha na kuweka sera bora za viwanda
kwa wawekezaji nchini, ambapo alitumia fursa hiyo
kutoa maombi maalumu kwa Mhe.Waziri Bashungwa.



“Tunakuomba wewe Mhe.Waziri kuweka msukumo
kwa watu wa bima BRITAM INSURANCE ambao
tulikata bima kwao waweze kutufanyia haraka
watulipe ili tuweze kununua mashine kufikia mwezi
julai mwaka huu kiwanda kianze kufanya kazi”.



Alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyo nayo kwa
upande wa viwanda wilayani Karagwe alifafanua
changamoto kubwa inayowasumbu mara kwa mara
kuwa ni tatizo la umeme ambalo limekuwa tatizo sugu
kwa wenye viwanda ambapo alisema kuwa kuna siku
umeme unakatika na kuwaka Zaidi ya mara 20 hivyo
husababisha kuungua kwa Motors,taa, na mitambo
mingine.



Kufatia kukithiri kwa matukio ya moto wilayani
Karagwe, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa wilaya
Godfrey Muheruka imeamua kujenga kituomcha zima
moto na uokoaji ambacho kitakuwa kikisaidia kwenye
ajali za moto pale zinapotokea.



Hata hivyo kitendo cha kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya ya karagwe kuamua kujenga jingo la zima moto
na uokoaji kikamshawishi waziri Bashungwa kuchangia
mifuko 200 ya saruji na kuwataka wadau wa maendeleo kuchangia ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa
wakati.

No comments