Ads

Mkurugenzi Manispaa Morogoro awaasa wazazi kutenga muda wa kutosha kukaa na familia zao.



akati dunia ikiadhimisha siku ya familia Duniani  leo Mei 15, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba ,amewaasa Wazazi na walezi  kutenga muda wa kutosha kukaa na familia zao ili kujadili, kushauriana na kutekeleza masuala muhimu ya kuendeleza familia zao; kwani familia ndiyo kitovu cha maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa leo Ofisini kwake Mei 15, 2020 katika maadhimisho ya Siku ya Familia duniani kwa njia ya Vyombo vya habari.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema Madhumuni ya Siku ya Familia Duniani ni kuhamasisha, kuhimiza, kuelimisha na kutanabahisha jamii kuhusu umuhimu wa familia katika jamii kwa nia ya kuchukua hatua zinazopasa ili kuziimarisha na kuziendeleza.

Aidha, amesema kuwa majukumu yanaongezeka siku hadi siku ambayo husababisha wazazi/walezi kufanya kazi siku zote za wiki na hata usiku, hatimaye kupunguza muda wa kukaa na familia hasa watoto wao na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa uwiano wa kazi na majukumu ya malezi.

Lukuba amesema, Pamoja na kwamba jamii zinatakiwa  kufanya kazi kwa bidii ili kukidhi mahitaji ya familia,lakini inabidi kuwianisha muda wa kufanya kazi na kukaa na familia ili watoto wapate malezi stahiki.

“ Familia nyingi tukizonazo ,  zinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mila na desturi zenye kuleta madhara, umaskini uliokithiri, mawasiliano na miundo mbinu mibovu ambapo husababisha hali ya maisha ya watu kuwa duni na tegemezi na hatimaye kutumia muda mwingi wa kufanya kazi bila ya kujali madhara yatakayotokea kwa familia, nitoe wito kwa ndugu na jamaa wanaoishi na watoto nyumba moja baada ya Wazazi wao kutoka kutafuta ridhiki  wawachukulie kama watoto zao na kuacha kuwafanyia vitendo vya ukatili, kipindi hiki Shule zimefungwa Watoto wetu wapo nyumbani isije shule zimefunguliwa badala ya kupokea wanafunzi tunapokea Wajawazito, ni matumaini yangu kwamba kupitia maadhimisho haya familia zitakumbushwa wajibu na mchango wao katika maendeleo ya familia zao, jamii na Taifa kwa ujumla “Amesema Lukuba.

Amesema madhara yanayoweza kutokea ni  pamoja na watoto kuwa na tabia mbaya kama kuacha shule, kukimbilia mitaani, kutokuwa na maadili na kuiga tamaduni zisizokubalika katika jamii yetu pamoja na mimba za Utotoni.



Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi wote Manispaa ya Morogoro kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hii kwa kuwa kila mmoja familia na ni sehemu ya familia ndani ya jamii.

Katika hatua nyengine, amesema maadhimisho ya mwaka huu yamelenga katika kuelimisha jamii hususani familia kujikinga na ugonjwa wa CORONA .

Amesema kutokana na ugonjwa huo na mikusanyiko ya watu , wametumia nafasi ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari.

Mwisho , amewataka a Wazazi na  Walezi Manispaa ya Morogoro kuwapatia kazi watoto nyumbani ili wasidhurure hovyo kutokana na janga la gonjwa wa COVID -19.

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe , amezitaka familia zizingatie maelekezo ya wataalamu wa afya katika kujikinga na Ugonjwa wa CORONA.

“ Wanafunzi wapo nyumbani, ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanatulia nyumbani na kusoma kwa  njia ya redio, TV na kufanya mazoezi ya mara kwa mara yanayotolewa na walimu wetu kwa njia ya vipeperushe” Amesema Mwanakatwe.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuwalinda na kuwaelimisha  watoto kuepuka mimba zisizotarajiwa ili watoto watakapo rudi shuleni wawe salama na waendelee na masomo yao ili wafikie malengo tarajiwa

No comments