Mitihani ya kidato cha sita sasa itaanza rasmi tarehe 29 Juni, 2020
Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako amesema Mitihani ya Kidato cha 6 itaanza Juni 29, na kumalizika Julai 16, 2020.
Amesema mitihani hiyo itaenda sambamba na ile ya Ualimu na kulitaka Baraza la Mitihani kuhakikisha wanasambaza ratiba inayoonesha mitihani itakavyofanyika.
Ndalichako ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa May 22 wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyoyatoa jana.
"Wanafunzi wa kidato cha sita watafungua tarehe 01/06/2020 kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli na wanafunzi watakuwepo shuleni wakijisomea na kufanya maandalizi ya mitihani mpaka tarehe 28/06/2020
"Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29/06/2020 na itafanyika hadi tarehe 16 Julai 2020, mitihani hiyo ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu
"Tumeliagiza Baraza la Mitihani la Tanzania kuhakikisha kwamba mitihani hii inapokamilika, ni lazima matokeo yake yatoke kabla ya Tarehe 31 Agosti,2020, ili tuweze kuendana na maelekezo ya Mhe. Rais kwamba wanafunzi hawa waweze kujiunga na vyuo vikuu "- Amesema Waziri Prof.Ndalichako.
Post a Comment