Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAANZA UTOAJI WA TUZO ZA USAFI KATA NA MITAA.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro ipo mbioni kuanza zoezi la utoaji wa tuzo za Usafi kwa Kata na Mitaa itakayofanya vizuri.

Akizungumzia  juu ya tuzo hizo,Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Morogoro  , Samwel Subbi, amesema wameamua kushindanisha Kata na Mitaa lengo likiwa kuweka Manispaa safi na kuleta hamasa kwa Watendaji wa Kata pamoja na Mitaa.

Amesema Moja ya matarajio makubwa ambayo yataleta mafanikio katika Kampeni ya Usafi ni pamoja na Viongozi wa Halmashauri kushawishi wananchi wake kuchangia ada ya taka kwa ajili ya ukusanyaji na uzoaji taka katika ngazi ya kata na Mitaa kwa ujumla.

Subi, amesema , mashindano hayo kwa upande wa ngazi ya Kata yatasimamiwa na  maafisa afya na watendaji yakilenga kusimamia zaidi  masuala ya  usafi na utunzaji wa Mazingira pamoja na jinsi ya kugeuza taka kuwa mali.
Amesema kuwa katika mashindano hayo vitatumika vigezo na mashindandano ambapo kwa kila robo mwaka mashindano hayo yatafanyika  na matokeo yake kuwasilishwa katika Baraza la Madiwani .
Vigezo vitakavyotumika ni pamoja na udhibiti wa taka ngumu, usafi wa barabara, mifereji, maeneo ya wazi, stendi  za daladala, udhibiti wa taka maji, usafi wa Masoko na Magenge, usafi wa Majengo ya biashara,usafi wa Taasisi, upendezeshaji wa Mazingira, udhibiti wa uzururaji wa wanyama, uwepo wa vyoo bora, udhibiti wa shughuli za uchafu na uharibifu wa Mazingira, usafi wa maeneo ya makaburi pamoja na udhibiti wa Kilimo cha mazao marefu katikati ya Mji.
“Baada ya uzinduzi wa Kampeni yetu ya Usafi , sasa tumeona ili tuweze kufanikiwa zaidi tutoe zawadi kama motisha kwa Kata na Mitaa itakayofanya  vizuri, lakini sio tu tuzo tutatoa  fomu zitakazojazwa na Maafisa wa Afya wa Kata jinsi walivyoshughulikia changamoto ya uchafu katika maeneo yao na fomu hizo zitawasilishwa kwa Afisa Mtendaji kabla ya kufika Manispaa kwa ajili ya ufuatiliaji, tunawaomba Watendaji , Maafisa afya , pamoja na Wananchi tushirikiane kikamilifu ili Kampeni yetu iweze kufanikiwa hatimaye na sisi Manispaa siku moja zije Manispaa nyengine kujifunza kwetu  “ Amesema Subbi.
Amesema zawadi hizo zinatarjiwa kutolewa siku ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani , hivyo Watendaji wote  kwa kushirikiana na Maafisa afya wanatakiwa kuwasilisha taarifa za Mitaa iliyofanya vizuri katika Kata zao ili timu ya Mazingira iweze kuzipitia na kuwapata washindi.
Katika hatua nyengine,amewaomba Maafisa Watendaji kushirikiana kikamilifu katika kuzuia katazo la Vifungashio vya palstiki ambavyo Serikali imepiga marufuku.
“”Kuanzia tarehe 1- hadi 15 mwezi Juni, 2020 tunaomba tuwasilishiwe taarifa Manispaa kwa Mitaa yote iliyofanya vizuri katika Kata, na sisi kuanzia tarehe 15 -25 mwezi Juni, timu yetu ya Wataalamu wataanza mchakato wa kuchuja na kuwapata washindi, ambapo washindi hao Kata zitatoka 3 na Mitaa 3, lakini suala zima la zawadi limebakia kwenye Kamati tutakapokamilisha mipango yote tutazitaja zawadi hizo” Ameongeza Subbi.
Kwa upande wa Afisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, ambaye ndiye katibu wa Kampeni ya usafi, amewaagiza Watendaji wa Kata kuwaelekeza Maafisa afya jinsi ya kuandaa mpango kazi katika Kata zao ili iwe rahisi kwa ajili ya ufuatiliaji.
Kipako, amesema tayari kuna wakuu wa Kanda za Kampeni ya usafi wameshapangwa na kilichobakia wanasuburia barua rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ili kuzishusha kwa watendaji waweze kuwafahamu na kushirikiana.
“”Tumejipanga vizuri, tangu tuanze Kampeni yetu kwa mara ya pili hii tumeanza katika Shule ya Msingi Mafisa A Kata ya Mwembesongo na Kata ya Mji Mkuu , tumeona kuna mwanga, nimeshuhudia baadhi ya maeneo yameanza kuimarika na yanaleta taswira nzuri sana, bado kuna changamoto ya wale wenye maeneo ambayo hawayaendelezi kuwa vichaka, tunatoa tamko wayafanyie usafi mara moja zaidi wakishindwa tutawapiga faini na kuwachukulia hatua kali za sheria, mwisho tunaombeni sana tutii sheria bila shuruti,  suala la kupigana faini sio jambo zuri sana , lakini na nyie wananchi mtoe ushirikiano kwa Viongozi wenu unapomuona mtu anatupa taka hovyo mpige picha au  toa taarifa tutamshurikia na kama kuna maeneo ni machafu  toa taarifa kwa Viongozi wenu tuyafanyie kazi tuanataka mji wetu uwe msafi na kuwa Halmashauri ya mfano hapa nchini  Amesema Kipako.
Mwisho, amewaomba Watendaji wa Kata kufuatilia kwa umakini fomu za usafi zinazojazwa na Maafisa afya kabla haizjafika makao makuu ya Idara,lakini niombe ushirikiano huu tuufanye sisi Kata,  Mitaa  pamoja na Maafisa wa Afya ili zoezi la Kampeni.

No comments