Ads

KAMPUNI YA FMJ HARDWARE LIMITED YAZINDUA MFUMO MPYA WA UUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI KWA KIDIGITAL






Meneja Mauzo Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited Bw. Fredrick Ally Sanga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited iliyopo Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam leo wamezindua mfumo mpya wa uuzaji wa vifaa vyote vya ujenzi vya nyumba na majengo kupitia njia ya mtandao (Online Media).

Vifaa hivyo vya ujenzi wa nyumba na majengo vinavyopatikana kwa ajili ya ujenzi kuanzia ngazi ya msingi hadi kumaliza nyumba kwa kutumia vifaa bora na venye viwango vinavyostahili.

Uuzaji wa huo wa vifaa vya ujenzi unafanyika kwa njia ya moja kwa moja mubashara kutokea katika kampuni ya FMJ Hardware Limited.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mauzo Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Limited Bw. Fredrick Ally Sanga, amesema kuwa lengo la mnada huo ni kumuwezesha mwananchi aweze kufikia ndoto zake za kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.

Amesema kuwa katika mnada huo kutakuwa na vifaa vya ujenzi bora venye gharama nafuu ambapo itakuwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha watu wanafanya kazi huku wakiendelea kujingika na ugonjwa wa homa kali ya mapafu corona.
“Mnada huu utasaidia kuepuka mikusanyiko katika kufanya biashara, ndiyo maana kampuni hii ya FMJ Hardware Limited ikaona ikufikishie na ikurahisishie wewe mwananchi kuagiza bidhaa zako utakazo hijitaji na kununua kwa njia rahisi kupitia mnada wa online media ukiwa umetulia nyumbani kwako ukifatilia pamoja na kufata kanuni za kujikinga na corona kwa kuepuka msongamano” amesema  Bw. Sanga.

Ameeleza kuwa mnada huo utaanza saa 6 mchana mpaka saa 9 alasiri ambapo utakuwa mubashara (live) kupitia online media ikiwemo Ayo Tv, Global Tv, Michuzi Tv, Tanzanite Tv, Dar Mpya Tv, Icon Tv, Javi Tv pamoja na vyombo vingine vya habari.
Hata hivyo Bw. Sanga amewakaribisha wananchi wote kufatilia mnada huo na kununua vifaa vya ujenzi kwa kupiga simu kupitia namba 0653 312 438, 0716 902 995 pamoja na kuwasiliana nao kupitia mtandao wa kijamii facebook Fmj hardware.

No comments