WAZIRI UMMY MWALIMU AMKABIDHI RC MAKONDA VIFAA VYA KUNAWA MIKONO KWAAJILI YA KUWAKINGA WANANCHI NA CORONA.aaa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Vifaa mbalimbali 350 vya kutakasa Mikono Ikiwemo Ndoo za Maji, Madumu, Masks na Dawa za kuchanganya kwenye Maji kwaajili ya kuwakinga wananchi dhidi ya Vimelea wa Virusi vya Corona.
Akipokea Vifaa hivyo RC Makonda amesemaa Vitapelekwa sehemu mbalimbali ikiwemo Vituo vya Daladala, Masokoni na sehemu zenye mzunguko wa watu ili Wananchi waweze Kusafisha mikono kabla ya kufanya jambo lolote.
Aidha RC Makonda amewaelekeza wakurugenzi wotewa Manispaa za Jiji hilo kuhakikisha Maji yenye Dawa hayamaliziki kwenye ndoo za kunawa mikono.
Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza Wananchi kuendelea Kuchukuwa tahadhari dhidhi ya Ugonjwa huo huku akiwaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa.
Msaada huo wa Vifaa 1,000 umetolewa na Mfanyabiashara Subash Patel chini ya Umoja wa Wafanyabiashara Wazawa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo kwa Dar es salaam wamekabidhi Vifaa 350 na Vifaa vingine 650 vilivyosalia vitasambazwa nchi nzima.
Post a Comment