TCRA Kanda ya Mashariki yatoa msaada kwa Kituo Cha Watoto Yatima
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto Yatima Cha New Home Orphan Kilichopo Boko Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Bi. Vaolet Eseko akimuwakilisha Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero, amesema kuwa wanatambua makundi maalum wanahitaji msaada ndio maana tumeguswa kuja kutoa.
Amesema kuwa TCRA kanda ya Mashariki imekuwa na utaratibu kutoa misaada mbalimbali katika kanda ikiwa ni wajibu wa mamlaka hiyo.
"Tumetoa msaada huu ili kuweza kuwasaidia kwa sasa na sikukuu ya pasaka pamoja na vitakasa mikono kwa kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona kwani dunia iko katika janga hilo" amesema Eseko
Hata hivyo amesema kuwa watoto wanatakiwa kuwa na furaha wakati wote kutokana na Jamii inayowazunguka kutambua matahitaji yao.
Mkurugenzi wa Kituo Cha New Home Orphan Mwanaisha Magambo, amesema kuwa anashukuru msaada huo na kutaka Taasisi zingine ziige mfano wa TCRA.
Amesema TCRA imekuwa ni mdau muhimu kutokana na kutambua mahitaji ya Kituo na kuwa hakuna udogo kwani mahitaji ya Kituo ni endelevu.
"Tunasukuru sana TCRA kuona umuhimu wa Kituo chetu kupata msaada wa chakula na vifaa vingine vikiwemo vitatakasa mikono na sabuni za kunawia kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona" amesema Bi Mwanaisha.
Post a Comment