CORONA YABADILISHA TARATIBU ZA USAFIRI DAR ,BAJAJI BODABODA SASA RUKSA KUINGIA MJINI
Mwamba wa habari
Kufuatia adha ya usafiri katika jijiji la Dar es salaam ulio sababisha na amri ya kuyaka mabasi ya abiria kubeba level siti ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 unaosababishwa na virusi vya CORONA mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe.Paul Makonda leo akizungumza na wananchi katika kituo cha mabasi ya makumbusho ameruhusu bajaji na Pikipiki (Boda boda ) kuingia katikati ya jiji ili kubeba abiria .
Pia Makonda amewaomba wamiliki wa nyumba,majengo ya ofisi na godauni kupunguza kodi hadi asilimia hamsini ili pesa ambayo itabaki wanunue chakula waweke ndani.
Vilevile amewataka wazazi kutulia nyumbani kama hawana safari za lazima ili kuepusha kusababisha maambukizi ya Corona kuleta nyumbani na kuathiri familia.
“Abiria tuwe walinzi wenyewe ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa corona wasijifiche kwaajili ya kuwakwepa askari wakati wanahatarisha maisha yao”amesema Makonda.
Nao baadhi ya abiria katika kituo cha mawasiliano amesema agizo la abiria kutokusimama kwenye daladala ni mwarobaini wa kujikinga na ugonjwa huo lakini ameziomba taasisi na mashirika ya umma kuwa na usafiri kwaajili ya kusafirisha wafanyakazi wao.
Wamesema usafiri umekuwa mgumu sana amefika toka asubuhi saa mbili lakini mpaka saa nne hajafanikiwa kupata usafiri.
Kwa upande wao makondakta katika kituo hicho wamesema ni janga ambalo hawajalitegemea pia abiria wanapata tabu hatakama gari likiwa limejaa wanalazimisha kupanda gari wakati serikali imeshakataza.
Post a Comment