WAZIRI KAMWELE ATOA SIKU 3 KWA LATRA KUSHAURI IDADI YA ABIRIA WATAKAOSIMAMA KWENYE MABASI YA MWENDOKASI

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko la wizara kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika huduma za usafiri wa umma ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya COVID-19(CORONA) leo jijini Dodoma
……………………………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Aridhini(LATRA) imetakiwa kukaa ndani ya siku tatu na Halmashauri za Majiji na Miji ili kuweka utaratibu maalumu utakaodhibiti wingi wa watu katika vituo vikuu vya mabasi ya masafa marefu kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya Virusi vya COVID-19(CORONA).

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika huduma za usafiri wa umma ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya COVID-19(CORONA).
Mhandisi Kamwele amesema kuwa LATRA kwa kushirikiana na wataalam wa afya, Shirika la ViwangoTanzania (TBS) pamoja na wadau wengine wakae chini ndani ya siku hizo ili kushauri idadi ya abiria watakaoruhusiwa kusimama katika mabasi ya mijini(daladalana mabasi ya mwendokasi.
Aidha Mhandisi Kamwele amesema kuwa madereva na makondakta wazingatie idadi ya abiria wa kusimama kwa mabasi ya mijini (daladala)kama itakavyo shauriwa na wataalam hao.
Hata hivyo Mhandisi Kamwele ameagiza Shirika la Reli Tanzania(TRC), Tanzania na Zambia (TAZARA), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) wahakikishe kuwa kunakuwa na vitakasa mikono(hand sanitizer) za kutosha katika maeneo yao ya kazi pamoja na ndani ya vyombo vyao vya usafiri kwa matumizi ya wasafiri na wanyakazi kama ilivyoagizwa na Waziri wa Afya.
“Pia katika hilo mamlaka hizo mnatakiwa kutenga vyumba maalumu kwa ajili ya abiria watakao bainika kuwa na dalili hizo ili vyumba hivyo viwezekutoa huduma ya kwanza huku taratibu nyingine za kuwafikisha sehemu ya tiba zikifanyika”, amesema Mhandisi Kamwele.
Pia Waziri amaezitaka mamlaka hizo kushirikiana na wataalamu wa wizara ya afya kuandaa matangazo na kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi kwenye vituo vya mabasi, malori, reli, bandari, vivuko, viwanja vya ndege pamoja na ndani ya vyombo hivyo vya usafiri kwa kutumia mfumo wa vipeperushi,mabango sauti na picha za kutembea (video).
Mhandisi Kamwele ametoa wito kwa watanzania kuwa iwapo kutabainika mtu yeyote mwenye kuwa na dalili za maambukizi ya virusi hivyo basi awasiliane na wizara ya afya kupitia namba za simu 0800110124 na 0800110125 kwa ajili ya kutoa taarfa kwa wataalamu wa afya pia namba hizo zibandikwe kwenye vituo vya usafiri na kwenye vyombo vya usafiri .

Post a Comment