Ads

MAWAKALA WA MELI NA FORODHA WAELEZA NAMNA COLONA AMBAVYO CORONA HUENDA IKAATHIRI BIASHARA .





Rais wa chama cha mawakala wa Forodha  Tanzania  Edward John Urio akizungumza na Mwamba wa habari kuhusu biashara ya  bandari na athari za Corona .



Mwenyekiti wa chamacha mawakala wa Meli Tanzania TASAA John Masawe akizunguza na mwamba wa habari

Na John Luhende
Mwamba wa habari
Rais wa chama cha mawakala wa Forodha  Tanzania  Edward John Urio ameipongeza serikali kwa kuchukua hatua muhimu katika kupambana na  ugonjwa hatari wa Corona na na kusema kuwa sekta ya usafiehaji wa mizigo melini bado ni salama .

Urio ameyasema hayo jijini Dar es salaa  na kuweka wazi kuwa pia athari za kibiashara bado hazijajitokeza kwani bandari ya Dar es salaam bado inainapokea meli ambazo zilipakia mizigo nchini  china tangu januri.

Kwa sasa sisi bado hatujapata athali tunatarajia siku za usoni kutakuwa na shida hiyo ,kwa sasa mizigo inayoshushwa hapa niile amabayo ilifungwa tangu na ksafirishwa tangau januari bado kunameli nyigi zina subiri kushusha mzigo"Alisema

Aidha ameishauri serikali  katika kuwanusuru wafanyabiashara na mtikisiko wa kiuchumi kwa kupunguza masharti na vigezo vya kufanya biashara katika matumizi ya Bank kwa wafanya biashara kutumia njia iitwayo Letter of Credit ( LC) .

"Hii nijia ambayo mfanyabiashara anaweza kutumia bank za ndani kuweza kufanya biashara na wafanyabiashara wengine Duniani  "Alisema.

Naye Mwenyekiti wa chamacha mawakala wa Meli Tanzania TASAA John Masawe amesema tangu ugojwa wa Corona kugunduliwa nchini China tahadhali ilikuchuliwa na hali ni salama na mizigo itaendelea kuingia katika bandari ya Dar es salaam.

"Utaratibu wa afya melini ni utaratibu wa kawaida kabla haija ondoka ama baada ya kufika nchi inakoenda lazima huwa wataalamu wa afya wanafanya upimaji kwa wanaoingia melini  kwahiyo bado ni salama"Alisema.

No comments