Ads

TCRA yawafunda Viongozi wa Dini Mkoa wa Kagera


Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustine Kamuzora ameiopongeza
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuja kwa  kampeni ya sirubuniki Mjanja Haingizwi Chaka.

Profesa Kamuzora ameyasema hayo wakati  akifungua semina ya Kamati ya Amani Mkoa wa Kagera  iliyoandaliwa na TCRA kutoa Elimu ya Kujikinga na uhalifu unapotumia  huduma za mawasiliano.

Katibu Tawala Profesa Kamuzora amewaomba  viongozi  wa dini  waunge  mkono  serikali kupitia  TCRA kueneza  elimu ya Mawasiliano.

 Amesema   viongozi wa dini Wana  wanawaumini wengi hivyo ni rahisi  kufikisha elimu hiyo.

"Ninaamini  viongozi wa Dini mkivalia  njuga  basi watu wataweza kujikinga na uhalifu wakati wanatumia huduma za mawasiliano"Amesema Profesa Kamuzora.

Naye Mkuu wa Kanda ya Ziwa Francis Mihayo amesema viongozi wa dini ni vizuri kuwa daraja ya kufikisha taarifa kwa haraka na watu.

Mihayo amesema  kuwa semina ya viongozi wa dini itazaa matunda kwa wananchi kuwa na uelewa namna ya kutumia mawasiliano.

Aidha amesema kuwa Kanda ya Ziwa itaendelea kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Kujikinga na uhalifu unapotumia huduma za mawasiliano.

Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania.

Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki Haingizwi Chaka.

Amesema wakati umefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.

No comments