Ads

TCRA yafikisha Kampeni ya Sirubuniki mjanja haingizwi chaka kwa viongozi wa Dini Morogoro.


Kamati ya Amani mkoa wa Morogoro imesema kuwa elimu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano imefika kwa wakati mwafaka kutokana na teknolojia hiyo kukua kila siku.

Wameyasema hayo wakati wa Semina ya Kamati ya Amani ya Mkoa  Morogoro inayotolewa na  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoa elimu juu ya utumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kujinga na Uhalifu unapotumia huduma hizo.

TCRA ipo katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja ambayo inakwenda katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani katika kutoa elimu hiyo utumiaji wa huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika Semina hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro Juma Ng'ondavi amesema kupata Semina ya huduma za mawasiliano kuna umuhimu kutokana na wao wanazunguka jamii yote ya Mkoa huo.

Amesema kuwa Kazi yao ni pamoja kuwa mabalozi kwa viongozi ambao hawajafika kuendelea kutoa elimu katika ibada ili waumini waweze kupokea elimu ya kujikinga na uhalifu wakati unapotumia huduma za mawasiliano.

 Katibu wa Makanisa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mkoa huo Mchungaji Canon Regnald Mdugi amesema  elimu waliopata TCRA wataipeleka kwa waumini kwa kuhakikisha wanaelewa katika kujikinga na uhalifu wakati kutumia mitandao ya mawasiliano.

Amesema viongozi wa dini kazi yetu ni kuitumia elimu hii na  kuipeleka  kwa waumini  kwa ustawi  wa nchi yetu

Kampeni ya  kuelimisha jinsi ya kujikinga na uhalifu wakati wa kutumia huduma za mawasiliano  ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Sirubiniki Mjanja  haingizwi  chaka  inayolenga  katika kuelimisha umma ya kujikinga.

Wakichangia  katika semina hiyo viongozi hao wamepongeza juhudi  za Mamlaka ya Mawasiliano za kuwalinda  wateja na kuahidi  kushiriki katika  kampeni  hiyo.

Kamati hiyo imetoa wito  kwa taasisi kuiga mfano  wa TCRA katika  kuelimisha viongozi wa dini wanawafuasi wengi  na ushawishi  mkubwa  katika   jamii.

Kampeni  ya Sirububiki  Mjanja haingizwi  chaka  imeandaliwa  na Mamlaka ya Mawasiliano  kushirikiana na Jeshi  la polisi  kitengo cha uhalifu  mitandaoni  yenye lengo la kuelimisha  jamii jinsi ya kujikinga  ili wasirubuniwe wanapotumia  huduma za mawasiliano.



 Kampeni  ya Sirububiki Mjanja haingizwi chaka  inalenga kuzifikia kamati za Amani za mikoa yote ya Tanzania.

Kamati za Amani za mikoa ni kamati za viongozi wa dini na madhehebu  mbalimbali ambazo zimeundwa kwa lengo  la kujenga  maridhiano kwa watu wa dini mbalimbali

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Christopher John amesema kuwa viongozi wa dini ni watu mhimu sana katika kutoa elimu kwa waumini.

Amesema kuwa huduma za mawasiliano ni pana na teknolojia yake inabadilika kila siku

John amesema TCRA itaendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya Mawasiliano kuhakikisha yanakuwa salama  kwa ustawi wa nchi.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa wanafikia makundi yote katika Kampeni ya Sirubuniki kuwa Mjanja.

Amesema wakati amefikia wa kutumia mawasiliano kwa kulinda usalama wa nchi  pamoja na wanaotumia mawasiliano bila kufuata sheria na taratibu mkono wa sheria utawakuta.

1 comment:

  1. Do you understand there's a 12 word phrase you can speak to your man... that will induce deep feelings of love and impulsive attraction to you buried within his heart?

    Because deep inside these 12 words is a "secret signal" that fuels a man's impulse to love, cherish and look after you with his entire heart...

    12 Words Will Trigger A Man's Love Impulse

    This impulse is so hardwired into a man's genetics that it will make him try better than ever before to take care of you.

    In fact, triggering this mighty impulse is absolutely important to having the best possible relationship with your man that the instance you send your man a "Secret Signal"...

    ...You'll soon notice him expose his soul and mind for you in a way he's never expressed before and he will recognize you as the one and only woman in the galaxy who has ever truly attracted him.

    ReplyDelete