Ads

SOMA HABARI ZA WHO KUHUSU ONGEZEKO LA WAGONJWA WA CORONA BARANI AFRICA .


Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa idadi ya watu walioathiriwa na virusi vya corona barani Afrika imepita watu 2,600.

Tedros Adhanom Ghebreyesus ameviambia vyombo vya habari kwamba, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani Afrika imefikia 2,650 na kwamba wagonjwa wasiopungua 49 miongoni mwao wameaga dunia.

Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema kuwa, shirika hilo liko tayari kuzisaidia nchi zote za Afrika na kuongeza kuwa: Nchi zenye mifumo dhaifu ya afya zinalazimika kuchukua hatua madhubuti za kudhubiti maambukizi ya virusi vya corona wakati zinapogundua kesi ya kwanza ya maambukizi ili kuzuia kusambaa zaidi virusi hivyo. 
 

No comments