Ads

RC MAKONDA -NI MAARUFUKU KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJITANGAZA KUWA UNA CORONA.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii vizuri na sio kutoa taarifa za uongo au kupotosha umma.
Kauli hiyo ameitoa  leo jijini Dar es salaam kwenye ziara yake katika kiwanda cha TRIDEA ambacho ni miongoni mwa viwanda vinavyo tengeneza vitakasa mikono kwaajili ya kujikinga dhidi ya virusi vya COVID 19 maarufu Kama Corona.
Pia amesema ni muhimu sana kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na sio watu huko mitandaoni ambao huleta hofu na kupotosha jamii.
“Kuna watu wamekuwa wajuaji sana huko kwenye mitandao ya kijamii ambao wanaleta hofu kwa wananchi niwaombe wana Dar es salaam na Watanzania kwa ujumla kila mmoja aamini Mungu yupo na kila mtu aombe kwa Imani yake mungu atuondolee ugonjwa huu”amesema Makonda.
Vilevile amewataka wananchi kusoma maelekezo punde tu wanapo nunua vitakasa mikono hivyo kabla ya kuvitumia isije ikawaletea madhara kiafya.
“Mwanachi pindi unapotumia vitakasa mikono usipeleke mikono kwenye macho au mdomoni pia mama weka mbali na watoto wasije wakapeleka mdomoni”amesema Makonda.
Sanjari na hayo amesema kuwa wameweka utaratibu wa kufatilia watu wote wanaoingia nchini ndani ya siku kumi na nne ili kubaini kama watakuwa wamepata maambikizi au la.
Hata hinyo Mganga mkuu wa mkoa Dk Rashisi Said Mfaume amesema ugonjwa huu unazuilika endapo wananchi watafuata ushauri wa wataalamu wa afya ambao ni kusafisha mikono kwa sabuni na maji yanayo tiririka na kutumia vitakasa mikono kwaajili ya kujikinga ili usipate maambukizi ya virusi hivyo.
“Tuepuke misongamano ambayo haina ulazima na tupunguze unyanyapaa na hofu dhidi ya virusi vya Corona ili kuepuka magonjwa mengine yasitupate”amesema Dk Mfaume.RC

No comments