Ads

MCHUNGAJI AFUNGUKA MAONO ALIYOPEWA NA MUNGU KUHUSU CORONA.


Mwamba wa habari
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona nchini na Duniani  mtumishi wa Mungu Mchungaji Evance Sindano amewataka watanzania kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi.

Mchungaji Sindano wa huduma ya MANIM  ministry , ametoa usahauri huo alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  ambapo amesema wakiwa katika maombi kama kanisa Mungu amempa mafunuo kwamba pamoja na usafi wa mwili watu  wanaoufanya wanatakiwa kuwa na usafi wa kiroho.

Aidha akizungumzia uponyaji wa Mungu alio oneshwa  mchungaji Sindano amesema .
''Mungu akanionesha watua wakimwamini watapona kwa jina langu wakiniamini na kwa kutumia asali,  asali hakuna mwanandamu atakaye jisifu kuwa ametengeneza dawa bali inetoka kwa Mungu  kisha akaniamba watanzania hawataangamia kwa ugonjwa huu  "Alisema

Pamoja na hayo Mchungaji huyo amewataka wafanyabiashara kuacha kuwapandishia  wananchi bei ya  bidhaa , pia asitokee mtu yeyote awe mtumishi atakaye sema anaichukua asali na kuiombea hapa kilamtu akiichukua popote alipo akaitumia  atapona.

No comments