Ads

BONDIA MWAKINYO KUZICHAPA NA BINGWA WA UJERUMANI MACHI 21.

Bondia wa Super Welter Weight Mtanzania Hassan Mwakinyo Tarehe 21 Machi 2020 anashuka ulingoni nchini Ujerumani kupigana na bondia Mjerumani Jack Culcay kuwania mkanda wa ubingwa wa WBO International Super Welter Weight.

Mwakinyo 24, ambaye katika uzito wa Super Welter anashika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika  na namba 20 Duniani , atakuwa ni bondia wa kwanza Mtanzania kugombea mkanda huo ambao ni wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Dunia wa WBO uliokuwa unaishikiliwa na bondia Manny Pacquiao.

Mpinzani wake Jack Culcay ni bondia namba 1 kwa ubora Ujerumani kwenye uzito wa Super Welter akishika nafasi ya 4 barani ulaya.

Jack Culcay ,34, amewahi kushinda medali za dhahabu katika mashindano ya ngumi Dunia, medali ya shaba katika Olympic na kumfanya kupatiwa jina la Golden Jack na Wajerumani.

Culcay ameweza kuutetea mkanda huo anaoushikilia mara moja dhidi ya Mjerumani mwenzake Jama Saidi .

Hassan Mwakinyo akifanikiwa kushinda mkanda huu na kuutetea mara mbili atakuwa amejiweka katika nafasi ya kugombea mkanda wa Dunia ambao umewahi  kushikiliwa na Manny Paquiao.

Mwakinyo mpaka sasa amepigana mapambano 18, akishinda 16 (11 kwa KO) na kupoteza mara mbili huku Mpinzani wa wake akiwa amepigana mapambano 31, na kushinda 27 (13 kwa KO) na amepoteza mapambano manne.

Mwakinyo anaenda pigana pambano hili akiwa na rekodi nzuri ya Kushinda mapambano yake mawili ya mwisho nje ya nchi moja dhidi ya Muingereza Sam Eggington na lingine dhidi ya Muargentina Raul Ginzalenz rekodi inayombeba dhidi ya mpinzani wake.

2 comments:

  1. Did you know there is a 12 word sentence you can communicate to your man... that will induce intense feelings of love and instinctual attraction to you buried within his heart?

    Because deep inside these 12 words is a "secret signal" that triggers a man's instinct to love, adore and guard you with his entire heart...

    ====> 12 Words Will Trigger A Man's Desire Instinct

    This instinct is so hardwired into a man's brain that it will make him try harder than ever before to make your relationship the best part of both of your lives.

    Matter-of-fact, fueling this dominant instinct is so important to achieving the best ever relationship with your man that the moment you send your man one of these "Secret Signals"...

    ...You will soon find him expose his heart and soul to you in a way he's never experienced before and he'll see you as the one and only woman in the universe who has ever truly fascinated him.

    ReplyDelete
  2. As claimed by Stanford Medical, It is in fact the SINGLE reason this country's women get to live 10 years more and weigh an average of 19 KG lighter than us.

    (And actually, it really has NOTHING to do with genetics or some secret diet and really, EVERYTHING around "how" they are eating.)

    BTW, I said "HOW", not "WHAT"...

    TAP this link to see if this brief questionnaire can help you discover your true weight loss possibility

    ReplyDelete