Ads

ANNA MAKINDA : BADO KUNACHANGAMOTO KWA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA UONGOZI.

Mwambawahabari

..........................

 Maria Kaira,Mwambawahabari

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda amesema bado kunachangamoto kubwa kwa Wanawake kuchangamkia  fursa za Uongozi katika ngazi mbalimbali Kutokana na hali ya uoga waliojiwekea.

Mhe. Anna Makinda ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, katika maadhimisho ya Miaka 25 ya Mkutano wa Beijing unaolenga kusherehekea mafanikio ya wanawake na kupanga mkakati wa kutetea haki za wanawake.

Amesema Tanzania haina haja ya kujisifia kuwa nchi ya Tano kuwa na wanawake wengi duniani kwa kuwa ni asilimia sita tu ya wanawake walio bungeni kati ya  asilimia 30 inayotambulika na Katiba.

Akizungumzia kuhusu ukatili wa kijinsia Mkurugenzi wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu LHRC Wakili Anna Henga, masema bado matukio ya ukatili yanaendele kuongezeka huku katika Miaka 25 ya Mkutano wa Beijing kumekuwa na ongezeko la vituo vya msaada wa kisheria ili kuwasaidia wanawake kupata haki zao za msingi.

Ameeleza sheria kandamizi kwa wamawake ni pamoja na mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 na 15, sheria ya Tamko la kimila pamoja na sheria ya mirathi huku akisema bado kuna mapungufu kwenye sheria ya kukataza ukeketaji kwa wasichana.


Hata hivyo, Mkurugenzi wa kituo cha Taarifa kwa Wananchi   TCIB Bw. Deus Kikamba amesema bado ametoa rai kwa wanawake kuwekeza kubomoa mfumo dume katika kuwahusisha wanaume katika mapambano ya usawa kwa wanawake.


Mkutano wa Beijing ulikuwa mkutano mkuu wanne kuhusu maswala ya wanawake uliolenga kutilia mkazo wa usawa wa kijinsia, Mkutano huo ulifanyika nchini China mjini Beijing, septemba 1995.

  

1 comment:

  1. According to Stanford Medical, It's indeed the one and ONLY reason women in this country get to live 10 years more and weigh 42 pounds lighter than we do.

    (And realistically, it has NOTHING to do with genetics or some secret-exercise and absolutely EVERYTHING to do with "how" they are eating.)

    BTW, I said "HOW", and not "WHAT"...

    Tap on this link to reveal if this short questionnaire can help you unlock your real weight loss possibilities

    ReplyDelete