Ads

MANENO YA MWISHO YA ALIYEKUWA WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KABLA YA KUWAJIBISHWA NA RAIS

Image result for picha za kangi

Na Mwndishi wetu
MANENO ya mwisho ya aliyekuwa Waziri wa Wizra ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola leo kabla ya kuwajibishwa na Rais, Dkt. Magufuli katika uzinduzi wa nyumba za Maafisa na Askari Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, leo.

Huku akiwa amevalia suti yake Nyeusi ya mikono mifupi akiwa ameshikilia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akitumia muda wa dakika nane kuongea 

Alianza kwa kusema Tanzania hoyeeeeee............

Magufuli hoyeeeee.......

Nani kama Magufuliiiii...... nani kama Magufuliiii....... ( huku akipunga mkono)

Mheshimiwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Mama yetu mama Janeth Magufuli,  Mke wa Rais, Mheshimiwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Mkuu wa Majeshi ndugu yetu Mabeyo, lakini kwa umhimu kabisa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye ametupa salamu za timu ya Yanga kule Singida, lakini niseme tuu kwamba  hata kule Singida walibaki na amani walioidumisha kutokana na kukubali matokeo ya kufungwa na Yanga.

 Kwahiyo amani watanzania tumefika mahala pale tunapofungwa wanatunza amani, Itifaki imezingatiwa.

Mheshimiwa Rais nianze na Jambo moja kwabisa la kuwakumbusha watanzania, juu ya kitabu hiki ambacho ni maarufu kwa jina la Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM),(Huku akipunga Kitabu cha Ilani ya CCM) kwaajili ya Uchaguzi wa 2015.

Mheshimiwa Rais kitabu hiki ni Mkataba baina ya chama cha Mapinduzi ibala ya pili pamoja na wananchi wapiga kura wa Tanzania.

Lakini Mheshimiwa Rais Kitabu hiki Ibala ya Nne wakati unazunguka nchi nzima, uliwaahidi watanzania kwa mujibu wa wa Ibala ya Nne.

Kwamba Serikali yako ya awamu ya tano itahakikisha kuna amani, itahakikisha kuna usalama, na utulivu wa hali ya juu na uliwahakikishia kwamba maisha ya wananchi pamoja na mali zao vitalindwa kwa nguvu zote za serikali.

Mheshimiwa Rais, naomba kwa unyenyekevu niuthibitishie Umma wa watanzania,mija wapo ya wizara ulizoziunda, katika kutekeleza jambo hili la amani, usalama na utulivu na maisha ya watu na mali zao ni wizara ya mambo ya ndani ya nchi.

Mheshimiwa Rais tukiwa tunawaambia watanzania, tukiwa tunawathibitishia watanzania, kwamba pamoja na n kwamba bado tunamuda mfupi wa kumaliza miaka mitano lakini Dkt. John Pombe Magufuli, ameweza kutekeleza ilani hii kuhakikisa nchi hii imetulia mahala pake.

Mheshimiwa Rais kulikuwa na matukio ya ujambazi wa kutumia siraha na bundukil leo mheshimiwa Rais imekuwa ni historia wananchi wanalala bila kusikia milio ya bunduki tumpigie makofi matatu Mheshimiwa Rais(Mhuku akiwa amenyanyua mikono juu kuashiria kupiga makofi).

Mheshimiwa Rais kulikuwa na ajali nyingi sana za barabarani lakini Mheshimiwa Rais uliendelea kutuhimiza wizara yako, na sisi tukasema hatutakuangusha, na ndio maana leo Mheshimiwa Rais ajali ambazo zinachukua maisha ya watu wengi pamoja na mali zao, sasa zinaenda ukingoni.

Na ndio maana Mheshimiwa Rais zamani tulifika pahala wananchi tukawa tunaogopa majambazi, kusafiri Nyakati za usiku, tulikuwa tunaogopa majambazi hata baadhi ya maeneo kwenda, tukafika pahala kana kwamba kwamba majambazi ndio yanapanga ratiba za watanzania, ni saa ngapi watakuwa watanzania watakuwa wanafanya kazi, tulifika pahala majambazi yakatupangia ratiba ya mabasi yasafiri saa ngapi na maeneo gani.

Mheshimiwa Rais nataka niuthibitishie Kwa niaba ya Serikali yako umma wa watanzania, leo mwananchi anauesafiri kutoka mikoa ya kaskazini anaenda Mbeya anaens Songea anasafiri anatoka Mikoa ya Dar ea salaam anakwenda kanda ya ziwa, Mwnza wanatoka Arusha leo wanasafiri bila wasiwasi masaa 24 makofi matatu kwa mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. 

Mheshimiwa Rais kumekuwa na maneno ya watu wanasema fedha ambazo unawaambia unakusanyabza kutosha kwaajili ya nchi hii na kwamba nchi hii umeipaisha sasa katika uchumi wapo watu ambao pengine pamoja na kwamba wanaona lakini hawataki kukubali matokeo nataka niwahakikishie kwamba ibara ya 146 (Huku akiwa wameishika juu Ilani ya Chama cha CCM)  katika  Ilani hii mambano ndogo tano uliwahakikishia watanzania kwamba vyombo vya ulinzi na usalama, utavipatia makazi kwaajili yabkujenga ari na morali kwa askari kwaajili ya kuendelea kulinda nchi hii amani na usalama wa nchi hii. 

Mheshimiwa Rais, nawathibitishia umma wa watanzania kwamba kama kuna wakati mheshimiwa Rais, umevisaidia vyombo vya ulinzi na Usalama kwenye eneo la makazi ni katika kipindi hiki, katika serikali yako ya awamu ya tano na ndio maana vyombo vya ulinzi na usalama iwe ni Polisi, kila kukicha majengo ambayo yanatupa fedha tunaendelea kuyazindua, tunakuwa na majengo ya uhamiaji, tunakuwa na majengo ya zima moto na leo Mheshimiwa Rais jeshi la magereza Tanzania, katika historia ambayo leo unaenda kuiandika, walikuwa na majengo duni, tangu mkoloni alipo acha jeahi la magereza hapa, hawakuwahi kuwa hata nyumba moja ya ghorofa, leo Mheshimiwa Rais umetujengea maghorofa ambayonumeandika historia, ambapo vijana wetu sasa wataenda kuishi na kufanya kazi kwa moyonmkubwa na ari kubwa. 

Na nimalizie kwa kusema Mheshimiwa Rais ilipotupatia fedha bilioni 10 kijenga makazi haya ya Askari yalikuwa yamelenga kujengamaghorofa manne katika nyumba moja ya brock moja lakini TBA walipokija hapa hatukuweza kutimiza azima hiyo, lakini naamini alipita hapa ibirisi shetani na jeshi lake, na ibirisi shetani alipokuja akakalia site, ndio maana TBA walikuwa na kigugumizi, kwa sababu walikuwa wamepigwa upofu, lakini Mheshimiwa Rais, wewe kama Amili Jeshi Mkuu ulipo tinga hapa ukiwa na majeshi mawili jeshi la Mungu pamoja na Jeshi lako lako ulinzi wa wananchinwa Tanzania na JKT, jeshi la ibilisi shetaniwaliweza kukimbia na kuiacha site, na ndio maana site hii ilikaliwa na majeahi yako na matokeo yake Mheshimiwa Rais tumeyaona ambapo leobunaenda kutukabidhi nyumba hizi na wale wanaoendelea kubeza juhudi zako Mheshimiwa Rais, wale ambaowanaona kwambabmacho yao hayaoni, lakini tunawaambieni, siku za serikali awamu ya tano zinafikia mwisho.

Watanzania wenye imani, watanania wenye moyo watanzania wanaokuunga mkono ni asilimia 99.1 ako 0.1ni wale ambao mioyo yao imeshikiliwa na adui shetani lakini na wao pia kwa jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai washindwe na walegee, na ninawafungua kwa minyororo ya upofu ili na hiyo asilimia waweze kukubali kazi unayoifanya.

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli namalizia kwa kusema kwa kuwa katika kipindi hiki watanzania wamekuweka juu ukang'araaa.... Ahaaa imekula kwao utaendelea kuwa juuuu tena juuu zaidi. Magufuli hoyeeeee.

Mheshimiwa Rais nakushukuru kaa nyumba hizi kama nilivyotangulia kusema, hatuna sababu ya kuendelea kuwa omba omba wa nyumba hizi kwa sababu Mheshimiwa Rais unasimamia miradi yetu, unaifahamu na uchungu nayo na ndio maana unaendelea kumwaga fedha na hizi fedha unazozimwaga kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, zile huduma wanazozitoa na matokeo ya amani na utulivu unaoona ndizo fedha za walipakodi zinazowafikia wananchi kwa njia ya huduma.

Na ninataka niwaambie watanzania, siku mkibeza juhudi hizi zinazofanywa  na kupitia amani ikakatika, usalama ukakatika  fedha zote Mheshimiwa Rais atazielekeza kununua malisasi, kununua mabomu kwaajili ya kulinda nchi, matokeo yake hatutajenga hospitali, watu hawatajenga shule, watu hawatalima na matokeo yake nchi itakuwa masikini.

No comments