Ads

Mamia ya wananchi mkoani Njombe wafurika NIDA



Na Amiri kilagalila-Njombe

Ikiwa ni siku ya mwisho kukamilisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole kwa kutumia vitambulisho vya taifa,mamia ya wananchi halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe  wamejitokeza katika ofisi za NIDA baada ya kukosa vitambulisho tangu walipojiandikisha mwaka jana.

Sababu inayotajwa na wengi kusababisha kukosa vitambulisho ni kuwa alama za vidole zimekuwa zikikataa kuonekana katika mashine za NIDA kutokana na shughuli za kilimo na ufundi ambapo watalazimika kusubiri utaratibu mwingine wa kujaza fomu maalmu.

“Mfano mimi nilikuwa nikienda kwenye zile mashine nikiweka vidole zinagoma,imefika wakati muda umeshafika tayari na vidole bado vinagoma lakini Nida wameniambia watapeleka taarifa sehemu husika ili nisaidiwe”alisema mmoja wa wananchi

Aidha msajili wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA  mkoa wa Njombe Godwin  Odoyo amesema kuwa wanapata changamoto katika siku za mwisho ambapo  wananchi wengi wanalalmikia kukosa vitambulisho huku akibainisha kuwa kuna baadhi wamekuwa wakitoa taarifa zisizo sahihi katika vituo vya kujiandikisha.

“Changamoto kubwa ni hasa kutoka kwa watu wa mitandao ni wale ambao alama za vidole hazisomi,lakini pia wakati mwingine tunabaini kwamba watu wanaweza wasiwe na taarifa huku wengine changamoto kubwa ni kukosea taarifa zao”alisema Godwn Odoyo

Odoyo amewataka mawakala wa simu za mkononi kuingiza taarifa za wateja kwa usahihi badala ya kuwatupia lawama nida tatizo ambalo amesema linatokanana mashine za mitandao kuzidiwa .

No comments