Ads

AFISA ELIMU DAR AONYA WANAFUZI WATOVU WANIDHAMU KUFUKUZWA SHULE.



Na John Luhende
Afisa Elimu mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameonya tabia ya wanafunzi wanao jihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwemo kuvuta bangi  na kuvizia walimu kuwapiga mitaani  kwamba vitendo hivyo havita fumbiwa macho watakaobainika watafukuzwa shule.

Kauli hiyo ameitoa alipofanya alipotembelea shule ya Sekondari Vingunguti  akiambatana na Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto , kuzungumza na na walimu na wanafunzi kufuatia  matokeo mabaya ya kidoto cha nne na chapili  2019  ambapo aliitaja sababu ya kufanya vibaya kwa shule hiyo kuwa ni nidhamu kwa wanafunzi na baadhi ya uzembe wa walimu.

''Pamoja na sababu zingine ikiwemo upungufu wa madarasa  lakini tatizo kubwa ambalo limetufikisha hapa ni nidhamu nataka lifanyiwe kazi ilishule hii matokeo yaweze kubadilika nidhamu na taaluma ni mapacha wanafunzi wakiwa na nidhamu walimu nao watakuwa na moyo wa kuwafundisha"Alisema 

Alisema  amepata taarikuwa katika shule hiyo kuna wanafunzi wanajihusisha na vitendo vya uvutaji bangi na kwamba amefika shuleni hapo kwaajili ya kutoa onyo kwa wate watakao kaidi kuachana na tabia hizo taratibu za kisheria zitafuatwa na watafukuzwa shule.

"Niwaombe sana wale ambao inasemekanaa mnavuta bangi naongea kwa nafasi ya mwakilishi wa  kamishina wa elimu ,kamishina ambaye anasajili shule na kufuta shule ambaye ametutungia sheria na kanuni mbalimbali ya namna ya  kuendesha shule lazima tuzingatie sheria hizo ,leo sitaki niwasimamishe ila siku nyingine nikija nikiambiwa bado wapo tutawaondoa"Alisema.

Aidha aliagiza kujengwa kwa uzio wa mabati ilikuzuia wanafunzi wanaopenya na kuvuja utaratibu washule na kutoa ole kwa Mwanafunzi ataye diriki kubomoa mabati hayo na kwa kuendekeza utovu wa nidhamu kuwa atachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanafunzi wapendeni walimu wenu kwa kufanya hivyo mtajenga mahusiano mazuri hatakama ni saanje ya masomo walimu wanaweza kuwasaidia kimasomo"Alisema .
Hata hivyo amewaonya wanafunzi wa kidato cha nne wasije wakajiona kuwa kwa kuwa wanamaliza wakifanya makosa hawatachukuliwa hatua za kisheria .

"Sheria haichagui hata kama umebakisha muda mchache kama huna nidhamu ukifanya kosa  utachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufukuzwa ,someni kwa bidii msiharakie maisha  popote mtakapokutana na Mwalimu akakuonya msikilizeni  haiwekani shule hii ina zero 117 hivi kweli hatuna uwezo wa kufaulu"Alihoji

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imeweka  elimu bure ili kuwa saidia watoto wa masikini  na kwamba inaendelea kuzifanyia kazi changamoto ndogo ndogo ikiwemo madarasa na  madawati ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi.

Kwaupande wake Meya wa Manispaa ya amewataka walimu hao kusimamia nidhamu bila kumuonea haya mtu yeyote  na kuwa na umoja .

"Sisi tutaenedelea kufuatilia  maendeleo ya shule hii natumaini mabadiliko,nyumba ambayo imegawanyika yaani lenu siyo moja lazima mabo hayataenda tukibaini hamna mabadiliko na hamna maelewano tyutachukua hatua''Alisema 

Nao baadhi ya Wlimu waliopata fursa ya kuzungumza walizitaja badhi ya changamoto zinazo wakwamisha kuwani pamoja na wingi wa wanafuzi, ushirikiano mdogo kutoka kwa wazazi , nidhamu kwa wanafunzi na mikakati ya kuwaadhibu wanafunzi wanaofanya makosa.


No comments