Ads

WAZAZI WATAKIWA KUENDELEZA VIPAJI VYA WATOTO


 Diwani viti maalumu katika Manispaa ya Temeke Fatuma shija,    akitoa hotuba katika mahafali ya  shule ya  awali (Achivement day care ) iliyopo mbagala Jijini Dar es salaam,
Baadhi ya Watoto wa shule ya Achivement Day Care wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani)

Na John Luhende
  Mwamba wa habari
Wazazi na walezi wametakiwa kiviendeleza vipaji vya Watoto wadogo kwa kuwapeleka shule ili Taifa liweze kupata viongozi na wataalamu watakao iendeleza nchi.

Hayo yamebainishwa na Fatuma shija, ambaye ni Diwani viti maalumu katika Manispaa ya Temeke alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali shule ya awali (Achivement day care ) iliyopo mbagala Jijini Dar es salaam ambapo aliwataka wazazi kuhakikisha wanawaendeleza watoto hao shukle ya msingi ,Sekondari hadi vyuo vikuu.

"Niwaombe sana mkawaendeleze hawa wamekunjwa wanagakli wabinchi msije mkawavunja huko wanajua kusoma na kuandika mkawakazanienie kujifunza elimu ya kujitegema "Alisema

Aidha shija aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuwafundisha vizuri watoto hao kwa jua kusoma kiswahili na kiingereza kuandika na kuhesabu na kusema kuwa kuna baadhi ya shule watoto wanamaliza bila kujua kusoma jambo ambalo linachangia kuaharibu watoto na kujikuta hawanamsingi bora wa kielimu.

Napenda nikupongeze Mwalimu mkuu kwa ubunifu na uthubutu wako wa kuanzisha shule hii nivijana wachache walio hitimu vyuo vikuu wasio na fikra za kusubiri kuajiriwa na kumtaka asibweteke kwa sifa hizo bali aendelea kuwa mbunifu na kuandaa watoto wengi zaidi.

Kwa upande wake Mratibu elimu kata ya Kiburugwa Julius Mbwaga , aliwataka Wazazi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa shule hiyo kwa kulipa ada kwa wakati ili walimu waweze kulipwa kwa wakati na wawe na moyo wa kuendelea kufundisha kwa ari.

"Mara nyingi huwa napita Achivement Day Care ,wanamazingira mazuri ya kujifunza Watoto wanakula chakula kizuri ,shule hii imesajiliwa kwa kuchukua Watoto wa awali 1044 wanacheti daraja A nawaomba Wazazi na wadau kuiunga mkono shule hii ili iweze kukua zaidi ,nazitaka shule nyingine zijifunze kupitia shule hii"Alisema

Awali mkuu wa shule hiyo Procovius Cyprian, akizungumza aliwataka Wazazi kuwapa urithi wa elimu Watoto wao na kuwapa imani kumjua Mungu ambapo alisema kuwa wakirithishwa imani na elimu Taifa litapata viongozi bora , na wataalamu bora .

"Watoto hawa ni Taifa la leo na la kesho nawaomba Wazizi endeleeni kuwale hatakama leo wamehitu hapa msiwaache waendelezeni, nawashukuru wazazi na kuwapongeza kwa kuichagua shule yetu"Alisema

Katika lisala kwa Mgenirasmi Watoto hao walielezea shule yao kuwa inayo mazingingira bora ikiwemo uzio unao wake usala kwao na utulivu wakati wa masomo

No comments