WAHITIMU CHUO CHA UANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO NZITO KATIKA UTENDAJI WAO.
Serikali imewataka Waandishi wa Habari nchini kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu katika kazi zao kwa kutanguliza uzalendo wa Taifa lao kwanza.
Kauli hiyo ilibainishwa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Juliana Shonza wakati wa Mahafali ya 24 Chuo cha Uandishi wa Habari DSJ kwa Wahitimu wa Ngazi ya Astashahada na Stashahada.
Amesema kuwa wapo baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa sehemu ya kuchochea uvunjifu wa amani kwakuandika habari zenye kuh amasisha uchochezi na zisizokuwa na maadili katika jamii.
Amesema waandishi wahabari wamekuwa ni watu wa muhimu sana katika Taifa lolote na inashika uhai wan chi hivyo wasipozingatia weledi na uzalendo katika kazi zao wanauwezo mkubwa wa kuhatarisha usalama wa nchi
Pia,amesema hatagemei wahitimu hao wanaenda kushangilia au kuandika vitu ambavyo vinaichafua Serikali jambo ambalo litakuwa siyo la kizalendo kwa kuwa Taifa hilo ni letu sote hivyo lazima wakatumie kalamu na sauti zao vinzuri kwa kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
Akichukulia mfano wa kukamatwa kwa ndege hivi karibuni amesema baadhi ya waandishi wanaaza kuichafua Selikali hivyo wamekuwa wakifurahia mabaya yanayo ikuta nchi yao kwa kusahau kwamba wenyewe ni watanzania.
Katika hatua nyingine Juliana amewataka Waandishi wa Habari wote wasio na weledi na taaluma ya kazi hiyo kwenda kusoma kwa kuwa sheria hiyo itaanza kufanya kazi mwaka 2021.
Amesema,Serikali imepitisha Sheria namba 12 ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inamtaka kila mwandishi wa habari awe na elimu ya angalau stashada ifikapo mwaka 2021.
Amesma kutokana na sheria hiyo hivyo kwa wahitimu wa Astashada ni vyema mkajipanga mapema kukidhi vigezo hivyo.
Juliana amesema,Lengo la sheria hii ni kuipa heshima tasnia hii ya uandishi wa habari na kuwaongezea thamani waandishi wa habari hapa nchini. mwanahabari angalau elimu ya kuanzia Diploma.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Selemani Shekonga,amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya wanafunzi kukosa sehemu ya kufanyia mazoezi ya vitendo pindi inapofika muda wa wao kufanya hivyo nje ya chuo.
Shekonga Amesema changamoto hiyo inaleta usumbufu hivyo amewaomba waajiri kufungua milango ya kuwapokea wanafunzi kwa ajili ya mazoezi kazini.
Amesema aliwatakwa wahitimu hao kuweza kutumia kalamu na sauti zao vinzuri kwa kuhabarisha umma pamoja na kukiletea heshima Chuo.
Shekonge aliiomba serikali kuweza kuangalia uwezekano wawanafunzi wa vyuo vya kati kupatiwa mikopo iliwaweze kujiendeleza kitaaluma kwa kuwa wapo baadhi ya wanafunzi wanashindwa kusoma kwa kukosa ada .
Post a Comment