WADAU WA USAFIRISHAJI KWANJIA YA MAJI WAFUNGUKA JUU YA TASAC.
Na John Luhende
Wadau wa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya Meli (Marinetime Agency) Wameishukuru Serikali kupitia taasisi ya TASAC kwa kuwashirikisha kabla ya kufanyika kwa mabadiliko na kanuni na sheria katika sekta ya usafirishaji .
Hayo yamebainishwa na Rais wa mawakala wa forodha Tanzania (TAFA) ndugu Edward John Urio katika mkutano ulio andaliwa na TASAC ambapo amesema ni mara ya kwanza kwa serikali kuwashirikisha wadau hao kwani kipindi cha nyuma walikuwa wanajulishwatu kuhusu mabadiliko hayo .
"Kupita TASAC wamekuja kwetu kwaajili ya kutaka maoni yetu kwenye kanuni zitakazo kuwa zinasimamia ile sheria na 14 ya kuundwa kwa TASAC mwaka 2017 itakayo kuwa inasimamia , kwa bahati mbaya sana wadau walikuwa hawajashirikishwa kwa mapana marefu kwenye sheria yenyewe na sheria hii ikaenda kufanyiwa mbadiliko mwaka jana na wadau hawakushirikishwa vizuri na kukawa na changamoto sana " Alisema
Alisema , amefurahishwa na kuanza kwa ushirikishwaji na kusema kuwa ni hatua muhimu na kwamba wadu wamechangia kwa kujiamini kwani wanania njema na nchi yao na wanaenda sawa na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya kutaka kuiona Tanzania inakuwa nchi ya viwanda .
Aidha aliongeza kuwa , mabadiliko hayo yanaathali kubwa kwanchi na yanawza kuikosesha nchi mapato ikiwa wenye meli watahama na kuacha kutumia bandari ama kufanya biashara na Tanzania ,kwasasa gharama zimekuwa kubwa katika tozo za mizigo zinatozwa na TASAC ukilinganisha na zamani ambapo mawakala wa forodha walikuwa wakifanya .
Pia kumekuwa na ucheleshaji wa mizigo , wateja wa mizigo exclusive mandate hawakuzoea kulipa Storage,pia mteja anaona usalama unapungua kwani kupitia mawakala wa forodha waliwajibika kulipa lakini hapa TASAC halipi chochote lakini kikwazo kikubwa ufinyu na upungufu wa vitendea kazi vya kupakua meli zimekuwa zikisubiri kwa muada mrefu.
"Wito wetu kama wadau serikali inapswa kuitisha kikao upya cha wadau kunamapungufu mengi nahii ni kwasababu ya wadu kutoshirikishwa ipasavyo kutakuwa na bei kubwa ya bidhaa mfanya biashara kama anatozwa bei kubwa itamlazimu kuongeza bei ili kufidia gharama hizo "Alisema .
Mbobezi wa masuala ya shipping ,Bwana Julius Nguhula alisema biashara ya Meli inaamiiko yake na hii biashara hakuna serikali hata moja duniani inayo fanya , kama sheria hii itaapitshwa na kuanza kufanya kazi itaenda kudhoofisha bandari ya Dar es salaa
"Tumeishauri serikali kwamba tunaomba tena watoe muda mwingine ili sisi wataalamu na waoefu wa kazi hizi kitaifa na kimataifa tuweze kutoa ushauri ,kwamba sisi tumeona ugumu huu , tumeona mikingamo hii na Serikali huwa inadanganywa hivi na kwamba Delivery oder fee haitakiwi , hii si kweli tozo hii inatozwa duniani kote "Alisema
Mbobezi huyo alitoa wito kwa Serikali kutimiza waliyo kubaliana kwamba sheria hiyo imekosewa kwa kuwa vile ambavyo wadau wanashauri havifanyiwi kazi vitu vinafanywa siri na wadau wanaletewa kubariki sasa wamesha waambia wakifanya hayo biashara itaanguka .
"Tuna mwamini Rais ,kama atapokea ushauri huu kwa uzalendo wake kwajinsi anvo wapenda watanzania na biashara ya Tanzania naamini kabisa sheria hii itabadilishwa ,Shipping Bussines itakaa peke yake na mdhibiti atakaa peke yake na mwisho wa siku tuunde mamlaka ya udhibiti wa usari wa maji au Serikali ifungue kampuni ya biashara ya Meli itakayo shindana na makapuni mengine kama ilivyo TTCL"Alisema
Kwa uande wake katibu mtendaji wa Tanzania Shipping Agency Associtiation (TASAA) Bw Abel Uronu , alisema kutokushirikishwa wadau hayo mabadiliko hayakuzingatia maslahi ya wadau zaidi ni kuwaumiza , wizara haikushirikisha wadau mabadiliko haya hadi yakaenda yaka pita leo ndo wanakumbuka wadau ,pamoja na kwamba Waziri kisheria ana mamlaka hayo lakini bila ya kushirikisha wataalamu kutoa madhara yake ni makubwa .
"Madhara ya exclusive mandate bila kuangalia upande wapili kwa wadau , moja ya madhara ni kwamba TASAC wamepewa mamlaka pekee ya wao kufanya uwakala wa meli bila kuhusisha sekta binafsi ,unapo wapa peke yao kufanya hizo kazi kuhodhi ni kuleta ukilitimba na ucheleweshaji wa mizigo hapa ana kazi ya udhibiti na bado ana fanya kazi ya kibiashara anakuwa na majukumu mengi huyo mkurugenzi ufanisi katika utendaji utapungua "Alisema .
Post a Comment