Ads

TUME YA USHINDANI YATAKIWA KUWEKA UWANJA SAWA KIUSHINDANI

Image result for PICHA VIWANDA NA BIASHARA WAZIRI BASHUNGWA

Na John Luhende
Mwamba wa habari
Waziri wa Viwanda na biashara Mhe. Inocent Bashungwa ameitaka tume ya ushindani nchini (FCC) kusimamia haki na kuto mpendelea yeyote ili kuweka uwanja sawa wa ushindani kibiashara.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya ushindani wa kibiashara duniani yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ambapo amesema taasisi hii ni muhimu sana kuhakikisha kuwa inasimamia biashara hali itakaoyo saidia kujenga uchumi kwa Taifa.

"Mkakati wa serikali ni kuziwezesha kampuni na viwanda vidogo vinakuwa na kazi hii inafanywa na tumehii kwa hiyo natoa rai msiangalie uwezo wa kifedha wa mtu toeni haki sawa ninyi muwe marefarii mnao mnatenda haki"Alisema.

Kwa uande wake mkurugenzi wa Tume hiyo Bw John Mduma , alisema tumeya ushindani nchi imekuwa ikisimamia sheria na wanakiuka utaratibu wamekuwa wakichukuliwa hatua za kisheria .
''Kimsingi wanaofanya makosa ya kiushindani tunawashitaki na kesi ikiendeshwa ikibainika watozwa faini ya kuanzia 5% ya mapato ghafi ya kampuni"Alisema.

Siku ya Ushindani Duniani imekuwa ikiadhimishwa na Mamlaka za ushindani Duniani kote kuanzia Mwaka 1980, wakati wa Umoja wa Mataifa uliporidhia na kukubaliana na kanuni za kuzuia mienendo potofu ya biashara.

Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya ushindani tangu mwaka 2015 ,lakini kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu inayoendana na masuala ya kiushindani yanayojitokeza kote Duniani ya " Kuhakikisha Ushindani Madhubuti katika Ukuaji wa Dunia ya Kimtandao."


 

No comments