TATIZO LA VIRIBATUMBO NA UDUMAVU KWA WATOTO DAR, WADAU WAFUNGUKA NA HII NDIYO PICHA KAMILI.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Wazazi na walezi jijini Dar es salaam wametakiwa kuzitunza familia zao kwa kuzipatia vyakula vya kutosha hasa mlo kamili ili kusaidia ukuaji kwa Watoto.
Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Wilaya ya Kigamboni Rachel Muhando katika semina ya Lishe iliyo andaliwa na mkoa wa Dar es salaam na kushirikisha manispaa zake ambapo alisema pamoja na serikali kutenga bajeti kwaajili ya lishe mzazi analojukumu la kulisha chakula bora familia yake .
"Unapo simama na kuitwa wewe Baba maana yake umetimiza majukumu yako katika familia yako,katika masuala ya lishe hakikisha wanakula vizuri wanalala vizuri na pia wanakwenda shule"Alisema
Aidha alifafanua kuwa Serikali imetenga shilingi 1000, kila mtoto chini ya umri wa chini ya miaka mitano lakini hiyo pesa hapei mzazi moja kwa moja kununua chakula bali hutumika katika kuwapa virutubisho vya lishe .
"Nisemina nzuri sana nami nazihimiza halmashauri zetu ziweze kutila mkazo suala la lishe kwa kutenga hizo pesa kwa uaminifu ili tuwawezeshe wataalam kuwafikia wananchi wengi zaidi walioko chini zaidi na kuwapa elimu juu ya unonyeshaji Watoto na kuwapaitia chakula bora, kupunguza udumavua na utapiamlo ili hatimaye tuwe na taifa lenye wataalamu na waomi wenye akili timamu ambao "Alisema.
Kwa upande wake Afisa lishe mkoa wa Dar es salaa Neema Kweba ,alisema mkoa huo una asilimia 20% ya Watoto walio pata udumavu na uzito pungufu kwa Watoto waliochini ya uzito pungufu 11.6% natatizo lingine 28% ya wanawake wenye umri wa kuzaa kati ya umri wa miaka 15-49 wana upungufu wa damu ambapo kitaifa 29% na wengine 48% wanakumbwa na tatizo la kiriba tumbo na uzito ulizidi .
"Mara baada ya kubaini hili sisi kama maafisa lishe tukishirikiana na wenzetu katika sekta mtambuka tumekutana kujadili ninamnagani sasatunaweza kuwasaidia wananchi kuepukana na tatizo la lishe duni"Alisema.
Aidha alisema kuwekeza katika lishe ili kujitengenezea watu bora watakao tusaidia kwenda katika uchumi wakati kama serikali yetu inavyo himiza , kikubwa tuanashauri Baba na Mama waende vituo vya afya wahudhurie clinic hiiitawasaida kupata elimu juu ya namna bora ya kutunza mimba na mtoto atakapozaliwa .
'Jambo la kuzingatia mtoto anajengwa katika kipndi cha miaka miwili yaani ndani ya siku 1000, huuni muda muhimiu wa kuwatunza ili ukuaji wao mwili na akili ufikie kiwango sahihi na sasa tunaweza kuwa na taifa la wataalamu watakao endeshaviwanda na kuwa na wataalamu wengi zaidi"Alisema .
Naye Neema Mwagasege ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki katika semina hiyo alisisitiza wazazi kutowapa watoto wadogo chini ya miezi 6 chakula chochote ama maji hii itasaidia Watoto kuto ugua magonjwa jambo ambalo litasaidia ukuaji wa mtoto.
Post a Comment